WILAYA YA HANDENI YAJIZATITI KTK UZALISHAJI WA CHAKULA.
Na Peter Mtulia.
WILAYA ya Handeni mkoani Tanga
imetangaza kuwa haitaomba tena chakula cha mtaada kutoka serikali kuu kwa msimu
ujao kutokana na matarajio ya kuvuna kiasi kingi cha mazao yakiwemo mahindi na
ufuta ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Hendeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ya kumtaka kila mwananchi kulima kwa bidii na kupanda kwa kufuata maelekezo ya wataalam.
Akiwa katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Manga, Kwamsisi, Kang’anta, Madebe, Misima, Sindeni, Mzeri na Mbagwi wilatyani Handeni, Mkuu huyo wa wilaya Bw. Rweyemamu alisema katika msimu ijao, wilaya hiyo haitaomba tena chakula cha msaada kwa vile wana uhakika wa kuvuna chakula cha kutosha.
Amesema pamoja na kwamba mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote zimekuwa zikileta madhara kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa wilaya ya Handeni mvua hizo zimeleta neema na faraja kwa wakulima kutokana na kuimarika kwa mazao yao mashambani.
Bw. Rweyemamu amesema karibu ya maeneo mengi wilayani humo, wamepata mavuno ya kutosha hasa mahindi na ufuta.
Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, amesema kuwa wakulima wengi katika wilaya hiyo wamelima kwa kutumia trekta na majembe ya kukokotwa kwa wanyamakazi jambo ambalo amesema litawaongezea ufanisi mkubwa msimu huu.
Na kwa upande wao baadhi ya wakul;ima wilayani humo wamesema chakula kitakachopatikana msimu huu wilayani humo hakijawahi kupatikana zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Post a Comment