Na Peter Mtulia, Tanga.
Halmashauri ya jiji la Tanga imetoa wito kwa wakazi
wake kupitia maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano mkoani hapa kuwa
wananchi wapate kutembelea banda lao ili waweze kupata taarifa sahihi kuhusu mji
wa Pongwe pamoja na mambo ya usafi wa Mazingira .
Hayo yamesemwa na
mwoenyeshaji wa maonesho haya kwa niaba yah alma shauri Juma Mkombozi wakati
akizungumza na redio huruma viwanjani
hapo kuhusu utoaji wa huduma yao kwenye maonyesho hayo ya kimataifa .
Aidha amesema kuwa
lengo la wao kushiriki kwenye maonesho ni kueleza kazi zao
na shughuli zote za halamashauri kwa wananchi ili wapate ufafanuzi juu ya mambo ambayo hawayafahamu .
Akielezea shughuli za halmshauri amesema kuwa ni pamoja na fursa
na maeneo ya uwekezeji yliyopo ktika jiji la Tanga na kutolea ufafanuzi wa
shughuli za wadau wa maendeleo ya
jiji.
Sanjari na hayo amesema wakazi wa jiji la hawana budi
kutambua kuwa halmshauri inendelea
kufanya jitihada zake kufanikisha kuwa Tanga Televisheni itaanza
kutumika baada ya muda mfupi
hivyo wananchi wameombwa kuwa na
subira.
Post a Comment