WAZEE MKOA WA TANGA WALIA NA USAWA

WAZEE MKOA WA TANGA WALIA NA USAWA




Na Peter Mtulia, Tanga.
 
BARAZA la wazee mkoani tanga limeiomba serikali kutunga sheria  ambayo itasaidia kuleta hali ya usawa, ulinzi  na usalama kwa wazee ili kuwaondolea changamoto  mbalimbali wanazokumbana nazo katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na katibu  wa umoja huo [TARINGO] mkoani hapa ferdolin mbunda wakati akizungumza na redio huruma ofisini kwake amesema kutokana na wazee wengi kutotendewa haki katika jamii serikali haina budi kuingilia kati suala hili kwa kuweka sheria za kuwajali wazee.

Aidha amesema serikali  itoe elimu kwa jamii ili iweze kujua umuhimu wa  wazee kwa kuwajali zaidi ki afya kwa kuweka vituo maalum ambayo yatasaidia  upatikanaji  wa matibabu kwa urahisi ili waweze kuepukana na foleni pale wanapofika mahospitalini.

Wazee hao wameiomba serikali iweke pensheni ya jamii na pensheni ya kawaida ambayo itasaidia wazee kupata huduma za matibabu kupitia maafao ya huduma hizo ili waweze kukidhi mahitaji yao.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger