DENGUE HAIPO TANGA.
Na Peter Mtulia.
WIZARA ya afya na ustawi wa
jamii, kupitia serikali Mkoani Tanga imekanusha madai ya yanayo enezwa wa
wananchi juu ya kuwepo wagonjwa wanaougua homa ya dengue mkoani hapa.
Akizungumzia uvumi wa
kuenea kwa ugonjwa huo Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga Asha Mahita, amewaambia
waandishi wa habari kuwa may 12 walipokea mgonjwa aliyeonesha dalili za ugonjwa
huo hatahivyo baada ya kufanyika vipimo ikaonekana hana ugonjwa huo.
Mahita amesema kuwa
hata baada ya kufanyika mawasiliano katika wilaya zote za mkoa wa Tanga tarifa
za kitabibu zimethibitisha hakuna mgonjwa aliyedhaniwa kuugua Dengue
Hata hivyo Mganga
mkuu amewataka wananchi kutosita kuchunguza afya zao katika vituo vya afya pale
inapoonekana dalili za ugonjwa huo na kutilia mkazo umuhimu wa kuendelea
kufanyIKa usafi wa mazingira ili kuzuia uwezekano wa mbu wa Aedes anaeambukiza
ugonjwa huo kuzaliana.
Post a Comment