SEREKALI YAOMBWA KUWASAIDIA VIJANA KUPATA AJIRA
Na Rose Sempeho
Kutokana na Vijana wengi kukosa Ajira
Serikali imeombwa kutoa fursa za Ajira kwa Vijana ili waweze kujikwamua
kiuchumi na kimaendeleo hali itakayopelekea vijana hao kutopotea kimaadili.
Rai hiyo imetolewa na Wafanyakazi wa Kampuni ya
Amboni Plantation,Deo Peter Mungia na Gauwa Nyumbwe katika mahojiano na Redio
Huruma jijini Tanga ambapo wamesema serikali itoe fursa kwa vijana ili waweze
kujikwamua na Umasikini na kujitenga na makundi hatarishi kamavile Wizi
Ujambazi na mengineyo ambayo hayaruhusiwai katika Jamii.
Aidha wamesema Vijana wawe mastari wa mbele
katika kufanya shughuli za halali ambazo zitawasaidia wao wenyewe kupata kipato
chao kwa njia ya halali kama matakwa ya Mungu yanavyosema.
Naye Bi Suzana Sinza ambaye ni mfanyakazi wa Halmashauri
ya jiji la Tanga kitengo cha Afya na kinga amasema ni wajibu wa kila kijana kujua umihimu wake
katika jamii kwa kufanya shughuli za kujitolea , kujitunza na kujithamini
katika kazi zao kwa kutambua wao ni nani katika jamii.
Sambamba na hayo amewataka vijana kutochagua
kazi bali kufanya kazi yoyote ile halali kwani wao ni wategemewa wakubwa katika
Taifa la kesho.
Post a Comment