Tanga Cement yaahidi kuendelea kudhamini Kili Marathon
Baadhi
ya maofisa wa kampuni ya Saruji Tanga (TCCL) wakishiriki mbio za mwaka
huu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi
Mkoani Kilimanjaro jana. Tanga Cement ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mbio
hizo ikitoa maji ya kunywa na kupoozea mwili kwa wakimbiaji.
Mmoja
wa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za Kilomita tano za Vodacom Fun
Run, Tsadia Jessie Bercuvitz (5) raia wa Uingereza akipewa sponji lenye
maji kwa ajili ya kupunguza joto na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Saruji
Tanga, Mtanga Noor wakati wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Premium
Lager Marathon mjini Moshi, Kilimanjaro juzi.
Waziri
wa Habari Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo ,Dkt Fenella
Mukangara akimpa cheti Meneja Mauzo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL),
Leslie Massawe (wa pili kulia) kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo
katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon
yaliyomalizika juzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. Kushoto kwa Waziri
Mukangara ni Waziri wa Mifugo, Dk Titus Kamani.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Saruji Tanga, Changwa Mjella (kulia) na Mtanga Noor
(katikati) wakimpa maji mmoja wa wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za
Kilimanjaro Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi,
Kilimanjaro juzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Reinhardt Swart (kulia)
akimpa maji mmoija wa wakimbiaji wa mbio za mwaka huu za Kilimanjaro
Premium Lager Marathon zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro
juzi. Tanga Cement ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mbio hizo ikitoa maji
ya kunywa na kupoozea mwili kwa wakimbiaji . Wengine ni maofisa wa
kampuni hiyo.
Post a Comment