KOCHA Mkuu wa Simba,
Zdravok Logarusic, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata
ili washinde katika mechi yao dhidi ya Prisons, mchezo unaotarajiwa
kupigwa kesho katika Uwanja wa Sokoine jiji mbeya.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
KOCHA Mkuu wa Simba,
Zdravok Logarusic, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata
ili washinde katika mechi yao dhidi ya Prisons, mchezo unaotarajiwa
kupigwa kesho katika Uwanja wa Sokoine jiji mbeya.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam juzi, Logarusic alisema timu yote inahitaji ushindi katika mechi yao hiyo,
hivyo jambo kubwa ni kuona vijana wake wanakuwa makini zaidi uwanjani.
“Tumepoteza pointi muhimu
katika mechi iliyopita kwasababu ya wachezaji kutotumia ipasavyo nafasi za wazi
wanazozipata, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limetugharimu.
“Naamini wakati huu
wachezaji wote wanafahamu jambo gani muhimu wanapaswa kufanya uwanjani kwa ajili
ya kuwapatia maatokeo mazuri, maana mpira ni mchezo wa makosa,” alisema.
Alisema kuwa kila mchezaji
anaweza kufunga anapokuwa katika nafasi mzuri ya kufunga na kuhakikisha nafasi
tatu za wazi wanazozipata moja wapo wanaibuka na ushindi.
Simba itashuka dimbani
ikiwa na kumbukumbu za kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya JKT Ruvu, uliochezwa
Jumapili iliyopita katika uwanja wa Taifa, mechi iliyowasononesha mashabiki wao.
Post a Comment