wanahabari nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo serikali na taasisi zisizo za serikali, wameobwa kutangaza na kuelimisha jamii mifano bora inayoonyesha jinsi mwanamke na msichana akipewa fursa na kuwezeshwa

Kuelekea  maadhimisho   ya  siku  ya  wanawake  duniani  tarehe  8 Machi,2014, wanahabari  nchini  kwa  kushirikiana  na  wadau  mbalimbali  ikiwemo  serikali  na  taasisi  zisizo  za  serikali, wameobwa  kutangaza  na  kuelimisha  jamii  mifano   bora  inayoonyesha jinsi  mwanamke na  msichana  akipewa fursa  na  kuwezeshwa



tanga-wananwake-5.gif




Na  Keneth Maganga, Tanga leo



Kuelekea  maadhimisho   ya  siku  ya  wanawake  duniani  tarehe  8 Machi,2014, wanahabari  nchini  kwa  kushirikiana  na  wadau  mbalimbali  ikiwemo  serikali  na  taasisi  zisizo  za  serikali, wameobwa  kutangaza  na  kuelimisha  jamii  mifano   bora  inayoonyesha jinsi  mwanamke na  msichana  akipewa fursa  na  kuwezeshwa  hutoa  mchango  mkubwa  sana  kwa  familia  yake  na  taifa  kwa  ujumla.

Ombi  hilo  limetolewa  na   Wizara  ya  Maendeleo ya  Jamii, Jinsia  na  Watoto  kupitia   katibu  mkuu  Anna  T.  Maembe  ambapo  amesema  kuwa  hilo  ndilo  lengo  kuu  la  kuadhimisha  siku  hiyo  na  kuongeza  kuwa  wanawake  ni  zaidi  ya  asilimia  50  ya  Watanzania  wote  kwa  hiyo  wakishirikishwa  ipasavyo  katika  shughuli  za  maendeleo  ni  dhahiri  mchango  wao  ni  mkubwa  sana.

Aidha  wizara  hiyo  imetoa  wito   kwa  mikoa  yote  kushirikisha  wananchi  na  wadau  wote  katika  kuadhimisha  siku  hiyo  kwa  namna  watakavyoona  inafaa  kwa  kuzingatia  kauli  mbiu ya  mwaka  huu  2014   isemayo   “Chochea  Mabadiliko  Kuleta  Usawa  wa  Kijinsia” Na  kuongeza  kuwa  kwa  pamoja  tunaweza  kushiriki  kujiletea  maendeleo  ya  familia  na  Taifa  kwa  ujumla.

Pamoja  na  hayo  wizara  imebainisha  kuwa  kila  mwaka  ifikapo  Machi  8  Tanzania  huungana  na  nchi  nyingine  wanachama  wa  Umoja  wa  Mataifa  kuadhimisha  siku  ya  wanawake  ambapo  madhumuni  ya  maadhimisho  hayo  ni  kutoa  fursa  ya  kupima  utekelezaji  wa  maazimio, matamko  na  mikataba  ya  kimataifa, Kikanda  na Kitaifa  inayohusu  masuala  ya  maendeleo  ya  wanawake  na  usawa  wa  jinsia .Na  huku  madhumuni  mahususi  ya  siku  hiyo  yakiwa  ni  kuhamasisha  jamii  juu  ya  umuhimu  wa  kutambua uwezo  wa  wanawake  katika   kuchangia  kuleta  maendeleo  endelevu, kuelimisha  jamii  kuhusu  jitihada  mbalimbali  zilizofanywa  na  serikali  na  wadau  katika  kuwajengea  uwezo  wa  kiuchumi  na  kijamii   ili  waweze  kushiriki  kikamilifu  kujiletea  maendeleo  yao , familia  zao  na  Taifa  kwa  ujumla.

Akifafanua  kuhusiana  na  kauli  mbiu  ya  mwaka  huu  Maembe  amesema  kuwa  ujumbe  huo  unasisitiza  kuhamasisha  na kuelimisha  jamii  kuhusu  umuhimu  wa  kuzingatia  masuala  ya  jinsia  katika  kupanga  na  kutekeleza  mipango  ya  maendeleo, sambamba  na  muelekeo  wa  maendeleo  kijamii, kitaifa  na  kimataifa,  Na  kuongeza  kuwa  unasisitiza  na  kuhimiza  kuandaa  na  kutekeleza  mipango  inayozingatia  ushirikishwaji  na  ushiriki  stahiki  wa  wanawake  na  wanaume  katika  kujiletea  maendeleo  yao.Huku  akisema  kuwa  maadhimisho  hayo  kwa  mwaka  huu  2014  yatafanyika  ngazi  ya  miko.

Sambamba  na  hayo  Maembe  amebainisha  kuwa   maadhimisho  hayo  pia  hutoa  fursa  maalum  kwa  Taifa, Mikoa, Wilaya  na  wadau  wengine  kupima  mafanikio  yaliyofikiwa  katika  kumwendeleza  mwanamke,Lakini  pia   na  kubainisha  changamoto  zinazowakwamisha  kufikia  azma  ya  ukombozi  na  maendeleo  ya  wanawake  na  kuweka  mikakati  ya  kukabiliana  na  changamoto  hizo.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger