WAHUSIKA... MNAIONA HALI HII?
Pichani
ni pipa la taka taka lililojaa uchafu karibu na mtaa wa chuo kikuu huria
kilichopo katika manispaa ya Iringa, pipa hilo lipo karibu na makazi ya
watu hali ambayo inaweza kupelekea mlipuko mkubwa wa magonjwa na
hatimaye kuathiri afya za watu.
Taka taka zilizomwagwika chini baada ya kukosekanika kwa nafasi ya kuzihifadhi katika pipa hilo zikiwa karibu na barabara itumiwayo na wakazi wa eneo hilo.
Pichani ni pipa hilo lililojaa uchafu ambao unatapakaa mpaka kwenye misingi ya nyumba za wakazi wa eneo hilo, hali hii ni ya hatari kiafya hasa kwa wakazi wa eneo hilo pia wapitaji.
jitihada za kumpata bwana afya wa manispaa hiyo hazikuzaa matunda hivyo msemaji mkuu wa kuelezea tatizo hilo hakuweza kupatikana kwa muda muafaka lakini jitihada za kuwapata wahusika wakuu wa eneo hilo bado zinaendelea.
Na Riziki Mashaka.
Post a Comment