Na Keneth Johni Maganga, Tanga leo
Imebainika
kuwa wananchi 7
kati ya 10
wanaamini mtu tajiri hawezi
kuadhibiwa kwa uhalifu
au kosa alilotenda.
Takwimu
hizo zimetolewa jijini
Dar es salaam na
mkuu wa Twaweza
Bw; Rakesh Rajani alipokuwa
akitoa muhtasari wa
utafiti wenye jina
la “JE, TUKO
SALAMA?” ambapo
wananchi 6 kati ya
10 ilibainika kuwa
wanaamini viongozi wa
dini, maafisa wa polisi, viongozi waandamizi
wa serikali na
viongozi wa umma
hawawezi kuadhibiwa kwa
makosa au uhalifu
wao.
Aidha
Rajani amesema kuwa
katika tafiti hiyo
wananchi walipoulizwa ni
kwanini watu hawaripoti
uhalifu kwa polisi, Watanzania walionekana kulaumu suala
la rushwa na
polisi kutowahudumia ipasavyo, ambapo takwimu
zilionyesha kuwa Mwananchi
mmoja kati ya
watano amesema kuwa
atalazimika kumlipa polisi
kiasi cha pesa
ili apatiwe msaada,na huku
idadi hiyo hiyo
ikisema polisi wasingewasikiliza au kuwajali
pindi wanapofikisha taarifa
kituoni.
Rajani ameendelea kusema
kuwa tafiti hiyo
pia ilichunguza mtazamo
wa watu kuhusu
mfumo wa sheria, ambapo kwa
hali ya kawaida watu
wanaporipoti uhalifu kwa
polisi, ni haki
yao kutarajia kuwa
polisi watajaribu kumkamata
mhalifu na kisha
kumfikisha mahakamani na hukumu kutolewa kwa
mujibu wa sheria. Lakini hali
ilionekana tofauti kwani
takwimu zilionyesha kuwa
Watanzania wana imani
ndogo kama hayo
yanatendeka. Huku nusu yao
(52%) wakiamini kama
mwananchi wa wakawaida
atafanya kosa au
uhalifu ataadhibiwa kwa
mujibu wa sheria,
jambo lililoashiria kutia
shaka, Halikadharika
wananchi pia walionekana
kuwa na mtazamo wa
kutokuwepo kwa usawa
mbele ya sheria
kulingana na hadhi
ya mtu.
Hata
hivyo takwimu za
tafiti hiyo zimeonyesha
kuwa wananchi wanapokumbana na uhalifu, wangependa kuripoti
polisi, ingawa ni nusu
tu ya wananchi
wote (47%) wanaofanya
hivyo na huku
idadi ikionekana kuwa
kubwa zaidi mijini
ambako watu 6
kati ya 10
(59%) waliripoti kuwa wangeweza
kuripoti uhalifu polisi, ikilinganishwa na
maeneo ya vijijini
ambako watu 4
kati ya 10 (39%)
pekee ndiyo wangefanya
hivyo. Ingawaje takwimu hizo zinaweza
kusababishwa na uwepo
wa polisi kwenye
maeneo ya mijini
kuliko vijijini.
Pamoja na
hayo Rajan amesema
kuwa takwimu za
tafiti hiyo zimeonyesha
kuwa vurugu katika
jamii hutokea kwa
wingi zaidi kuliko
wizi, ambapo Februari 19,2014
Dar es salaam karibu
nusu (46%) ya
watanzania wote wamearifu
kuwa wameshawahi kushuhudia
vurugu katika jamii
ndani ya kipindi
cha miezi sita
iliyopita, ikilinganishwa na idadi
ya mtu mmoja
kati ya watano
anayeripoti kuwa amewahi
kuibiwa kitu na
wezi,Na huku nusu
ya watanzania wote
wanaripoti kuwa hawajawahi
kuibiwa kitu, halikadharika watu
wanne kati ya
kumi ndio hawajawahi
kushuhudia vurugu au ghasia
katika jamii.
Post a Comment