Khamis Tambwe mabao aumwa tumbo ghalfa

Khamis Tambwe mabao aumwa tumbo ghalfa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
DAKTARI wa timu ya Simba, Yasin Gembe, amesema mshambuliaji wao Khamis Tambwe, amepata mvurugiko wa tumbo hivyo kukosa kufanya mazoezi ya asubuhi na wenzake.
Muda wote wa mazoezi, Tambwe alikuwa nje ya uwanja, hivyo kuzua hofu kwa wadau na mashabiki wa timu ya Simba wanaokoshwa na kasi ya mshambuliaji huo ndani ya uwanja.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Gembe alisema kuwa mshambuliaji wao Tambwe aliamka vibaya kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya ghafla ya tumbo.

Alisema hata hivyo maradhi hayo si tatizo la kumfanya asiwe mzima kwa siku mbili na kuongeza kuwa afya yake itatengemaa haraka kwa ajili ya kuwapo uwanjani mwishoni mwa wiki pale timu yake itakapovaana na Ruvu Shooting, Jumamosi, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
“Tambwe anaendelea vizuri baada ya kupata tatizo la kuumwa tumbo, ila hali yake haitampa wakati mgumu kuingia uwanjani kucheza na timu ya Ruvu Shooting Jumamosi katika Uwanja wa Taifa.
“Mbali na Tambwe, pia majeruhi Henry Joseph na Issa Rashid wote wamepona na wameanza mazoezi jana na wenzao, hivyo nadhani hii ni hatua nzuri kwa Simba,” alisema.
Mechi ya Simba na Ruvu Shooting inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa Simba, wenye hamu ya kuona timu yao inaendelea kufanya maajabu kwa kushinda ili ijiweke katika nafasi nzuri kileleni.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger