TFF wasaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni ya Azam kwa ajili ya kuonyesha mechi za ligi Kuu
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu)
wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights)
utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Rais wa TFF. Leodgar Tenga
Mkataba huo wa miaka
mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya
TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa
kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi Kuu ya Tanzania
sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa
na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati
wowote kuanzia mwezi ujao.
Post a Comment