Jamii
imeaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi badala ya kuwaona ni kama
maadui kwao hasa wanapofuatilia taarifa za uhalifu ili kuhakikisha wanashirikina katika kulinda na kuzuia vitendo vya kihalifu vinavyofanyika miongoni mwa jamii .
Ushauri huo umetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe wakati wa
maadhimisho ya siku ya polisi ambapo kwa mkoa wa Tanga wameadhimisha
kwa kutembelea kituo cha waathirika wa madawa ya kulevya SOBAR HOUSE pamoja na kituo cha kulelea watoto yatima na kutoa misaada ya kijamii.
Alisema jamii imekuwa ikilichukulia jeshi hilo kama sehemu ya maadui jambo ambalo sio kweli kwani nia
ya uwepo wao ni kuhakikisha wanalinda mali za wananchi pamoja na kuzuia
uhalifu wa aina yoyote usitokee miongoni mwa jamii na taifa kwa ujumla.
“Lengo
la maadhimisho ya siku ya polisi ni kufanya kazi ambazo zitaonyesha
tupo karibu na jamii ikiwemo kama kufanya usafi kwenye hospitali kwa Tanga tumeamua kutembelea ndugu zetu walioathirika na madawa ya kulevya pamoja na watoto yatima “alisema Kamnda Massawe.
Awali
akiwa SOBAR HOUSE aliwataka waathirika hao kuhakikisha hawarudi tena
kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kupona na kuwahamasisha
wenzao kutotumia madawa hayo kwa kuwaeleza madhara yatokanayo na
matumizi ya dawa hizo
“Nawaomba
baada ya kupona msikubali kurudi tena kwenye utumiaji wa madawa hayo
kwani yanarudisha nyuma maendeleo yenu na taifa kwa ujumla kwani mnapoteza muda mwingi kwenye matibabu yake na nguvu kazi ya taifa inapotea bure”aliwaasa Kamanda.
Hata hivyo akiwa kwenye kituo cha watoto yatima cha Abdillah bin Omari aliiasa jamii ya wanatanga kutowatenga watoto hao bali kuwatambua ni sehemu yao kwa kuwaonyesha upendo ili wajiihisi nao ni wajamii kama wengine
Jumla
ya msaada wenye thamani ya sh Laki saba ulitolewa kwa vituo hivyo
ikiwemo fedha taslim sh laki tanona katoni nne za maji ya matunda kwa kituo cha SOBAR HoUSE pamoja na mchele kilo 50 ,mafuta ya kupikia lita 10 na maji ya matunda katoni sita kwa ajili ya kituo cha Abdi Abdulrahmani
Post a Comment