Francis Cheka amtandika Mmarekani Phil Williams Ukumbi wa Diamond Jubilee na kuwapa raha Watanzania
BONDIA wa Tanzania, Francis Cheka, ameendeleza ubabe wake
baada ya kumtandika mpinzani wake Phil Williams katika pambano lao
lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar
es Salaam.
Bondia wa Tanzania, Francis Cheka, pichani
Ushindi huo wa Cheka ni furaha kubwa kwa Watanzania wote,
hususan wale wanaotokea mkoani Morogoro ambapo mkali huyo ndipo anapotokea
kwenye mji huo.
Cheka alipata ushindi huo na kunyakua ubingwa wa Dunia wa
WBU, baada ya kumpiga Williams kwa pointi kuonyesha kuwa yeye ni mkali na hana
mpinzani hapa Tanzania.
Mbali na kufanikiwa kumchapa Mmarekani huyo, mara kwa mara
Cheka amekuwa akiibuka na ushindi kila anapoingia ulingoni kupambana na
mabondia wa Tanzania.
Post a Comment