Featured Post Today
print this page
Latest Post

ARSENAL RAHAAAAAAAA, WENGER ASHEREHEKEA MIAKA 17 KAZINI KWA USHINDI WA UGENINI LIGI KUU ENGLAND

ARSENAL RAHAAAAAAAA, WENGER ASHEREHEKEA MIAKA 17 KAZINI KWA USHINDI WA UGENINI LIGI KUU ENGLAND

Happy days: Arsenal youngster Serge Gnabry celebrates after breaking the deadlock at the Liberty Stadium
  Happy days: Arsenal youngster Serge Gnabry celebrates after breaking the deadlock at the Liberty Stadium
 
 MFARANSA Arsene Wenger amefurah miaka 17 ya kuwa kazini kama kocha wa Arsenal kwa ushindi wa mabao 2-1 katika Ligi Kuu ya England leo dhidi ya Swansea Uwanja wa Liberty.
Shukrani kwao, Aaron Ramsey na kinda Serge Gnabry waliofunga mabao hayo, huo ukiwe ushindi wa 12 mfululizo kwa Gunners katika mashindano yote.
Swansea ilipata bao lake kupitia kwa Ben Davies dakika ya 82, baada ya Gnabry kufunga dakika ya 58 na Ramsey dakika ya 62.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny; Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Ramsey, Gnabry/Arteta dk77, Ozil/Monreal dk88, Wilshere/Jenkinson dk90 na Giroud.
Swansea: Vorm, Tiendalli, Flores, Amat, Davies, Canas, De Guzman, Dyer, Shelvey/Bony dk60, Routledge/Pozuelo dk64 na Michu.
 
 
Drilled home: Aaron Ramsey rifled in the second goal from close range as Arsenal doubled their lead
Drilled home: Aaron Ramsey rifled in the second goal from close range as Arsenal doubled their lead
No entry: Mathieu Flamini (left) shoots past Jose Canas but can't find the net
No entry: Mathieu Flamini (left) shoots past Jose Canas but can't find the net
Hard graft: Michu flies in to a tackle with Flamini as the Swans worked hard
Hard graft: Michu flies in to a tackle with Flamini as the Swans worked hard
On target: Gnabry celebrates scoring his first Premier League goal for Arsenal
On target: Gnabry celebrates scoring his first Premier League goal for Arsenal
No! Michu is not happy with a refereeing decision and falls to his knees
No! Michu is not happy with a refereeing decision and falls to his knees
Roar of delight: Olivier Giroud and Jack Wilshere (left) celebrate with Gnabry (obscured, centre)
Roar of delight: Olivier Giroud and Jack Wilshere (left) celebrate with Gnabry (obscured, centre)
Steered home: Gnabry watched his shot fly past Michel Vorm and into the net
Steered home: Gnabry watched his shot fly past Michel Vorm and into the net
Height mismatch: Nathan Dyer tries to trick his way past Per Mertesacker
Height mismatch: Nathan Dyer tries to trick his way past Per Mertesacker
Hunted down: Olivier Giroud is tracked by Jonjo Shelvey as he tries to make progress
Hunted down: Olivier Giroud is tracked by Jonjo Shelvey as he tries to make progress
Top of the league: Arsene Wenger saw his charges usurp Tottenham at the head of the Premier League
Top of the league: Arsene Wenger saw his charges usurp Tottenham at the head of the Premier League
Artist: But Mesut Ozil was not at his best as Arsenal won the game
Artist: But Mesut Ozil was not at his best as Arsenal won the game
0 comments

Hapa ndio stend ya mabasi ya Handeni Mjini

Hapa ndio stend ya mabasi ya Handeni Mjini



Hapa ndio kituo cha mabasi cha Handeni Mjini kama kilivyopigwa picha hii juzi wilayani humo mkoani Tanga. Ni tofauti na kituo cha mabasi cha Korogwe Mjini, Handeni hali inaonekana kuwa tulivu na hakuna mkanyagano sana. Hii ni kwasababu Mabasi mengi yanayopitia hapo yakitoka Tanga, Dodoma, Dar es Salaam hivyo kukusanya watu wengi mno. Picha na Kambi Mbwana.
0 comments

DC RWEYMAM AWAPA SOMO WAZAZI TANGA.

DC RWEYMAM AWAPA SOMO WAZAZI TANGA.

NA OSCAR ASSENGA,TANGA
MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweymam amewataka wazazi na walezi Mkoani hapa kuchangia kupatikana kwa unywaji wa maziwa shuleni ili kulinda afya na uelewa wa wanafunzi darasani.

Akizungumza katika siku ya unywaji wa maziwa Duniani na kufanyika kitaifa Mkoani Tanga, Rweymam alisema kinywaji hicho ambacho pia ni chakula ni muhimu kwa faida ya wanafunzi hasa kujenga afya zao.

Alisema wazazi wako na wajibu wa kuona kwa dhati unywaji wa maziwa shuleni ni muhimu na hivyo kuwataka kuchangia ili kuwezesha upatikanaji wa maziwa sambamba na uji shuleni.

“Ni jukumu la wazazi na walezi kuona unywaji wa maziwa shuleni ni muhimu ---mimi nadhani ni jukumu letu sisi wazazi kuwezesha upatikanaji wa maziwa na tusiwe na uzioto wa jambo hilo” alisema Rweymam

Rweymam alisema kufanya hivyo kutawawezesha wanafunzi kuwa na afya nzuri na kuzidisha uelewa darasani lengo ni kuwa na vijana wenye vipaji ambao watakuwa msaada kwa taifa.

Akifunga maadhimisho hayo, Naibu Meya wa jiji la Tanga, Muzzamilu Shemdoe, aliwataka wanafunzi kujibidiisha na masomo yao darasani pamoja na kuacha utoro jambo ambalo linaweza kuwaathiri na maisha mbeleni.

Alisema kuna baadhi ya wanafunzi wamekuwa hawafiki mashuleni mbali ya kuondoka majumbani kwao kuaga kwenda shule hali ambayo baadhi ya shule imekuwa ikikabiliwa na changamoto hiyo.

“Leo ni siku ya unywaji wa maziwa Duniani na kitaifa ni hapa tulipo---sisi tuliopo tu we mabalozi wa elimu majumbani na mitaani kwetu na tuhakikishe kila mtoto anakwenda shule na kuacha utoro” alisema Shemdoe

Shemdoe alisema halmashauri ya jiji inatarajia kufanya kampeni ya kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule haki hiyo anaipata na kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wao na kupata elimu.

                 
0 comments

WANAWAKE SINGLE WAANDAMANA KUSHINIKIZA SEREKALI IWASAIDIA WAOLEWE.

WANAWAKE SINGLE WAANDAMANA KUSHINIKIZA SEREKALI IWASAIDIA WAOLEWE.

Amini usiamini Nigeria ina upungufu wa wanaume wa kuoa!! Kiasi kwamba wanawake wanaotamani kupata wenza na kutengeneza familia wameamua kuchukua hatua.Zaidi ya wanawake elfu 8 walio single jana wameandamana kutokana na upungufu wa wanaume wa kuwaoa.


Lengo la maandamano yao ni kuishinikiza serikali kuwasaidia waolewe, kivipi? (Ndio swali hata mimi nimejiuliza!)

Wanawake waliojikusanya na kuandamana ni mkusanyiko wa 5380 waliopewa talaka, 2200 ni wajane 1200 yatima, na 80 wengine. Wanawake hao wamedai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku kwa sababu hawana wanaume wa kuwasaidia ndio maana wanahitaji wanaume wa kuwaoa na kuwasaidia mahitaji yao.
0 comments

BABU WA LOLIONDO ATABIRI"HIVI KARIBUNI TANZANIA ITAKUWA KIOO CHA AFRIKA NA DUNIA"

BABU WA LOLIONDO ATABIRI"HIVI KARIBUNI TANZANIA ITAKUWA KIOO CHA AFRIKA NA DUNIA"

 
MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapila ‘Babu wa Loliondo’ amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na baadaye kioo cha dunia.

 Ametoa kauli hiyo Septemba 24, mwaka huu mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha. 

Mchungaji Mstaafu Mwaisapila aliyesifika kwa tiba ya kikombe cha dawa, alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia na hayakutokea Israeli sasa yatafanyika Samunge. “Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nimeyaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa. 

Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameonyeshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa ‘kugawa kikombe’ ikiwemo mahema, maji na ulinzi. Pamoja na maono hayo aliyopewa Babu wa Loliondo, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT), marehemu Moses Kulola alikuwa akimpiga waziwazi katika mahubiri yake akidai mwenendo wa tiba alizokuwa akizitoa hazifanani na mafundisho ya Mungu. 

Kama hiyo haitoshi, watumishi mbalimbali wa Mungu wamekuwa hawamuamini. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ kwa nyakati tofauti waliwahi kunukuliwa wakisema hawana imani na tiba ya kikombe iliyokuwa ikitolewa na Babu wa Loliondo



0 comments

NGASSA ALIVYOWASILISHA MILIONI 45 ZA SIMBA TFF SIKU YA IJUMAA JIONI

NGASSA ALIVYOWASILISHA MILIONI 45 ZA SIMBA TFF SIKU YA IJUMAA JIONI


Mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa (katikati) akiwa ameshika risiti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kulipa Sh. Milioni 45, alizotakiwa kuilipia klabu ya Simba SC. Wengine kulia ni Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto na kushoto Mhasibu, Rose Msamila. Ngassa alifungiwa mechi sita za mashindano na TFF pamoja na kutakiwa kurejesha fedha za Simba Sh. Milioni 30 na fidia ya Sh. Milioni 15, baada ya kubainika alisaini timu mbili, Simba na Yanga alikoidhinishwa kuchezea msimu huu.

Ngassa akiwa ndani ya ofisi za TFF wakati anaandikiwa risiti baada ya kulipwa fedha

Ngassa akionyesha cheki alizokwenda kulipa TFF

Wapambe; Wanachama wa Yanga, Kaisi na Shamte kushoto walimsindikiza Ngassa leo

Risiti ya TFF

Cheki za Milioni 45
0 comments

Wengine wanasoma shule za gharama na wenzao wana choma mkaa, ajira za watoto zipo kwa wingi hapa nchini serikali ijitathimini upya kuhusu hili.

Wengine wanasoma shule za gharama na wenzao wana choma mkaa, ajira za watoto zipo kwa wingi hapa nchini serikali ijitathimini upya kuhusu hili.



Mtoto ambaye hajaweza kupatikana jina lake mara moja akijishughulisha na kazi ya uchomaji mkaa, kama alivyokutwa maeneo ya Kwachaga, wilayani Handeni mkoani Tanga. 
Mtoto kama huyu anastahili kutumia muda mwingi kusoma na sio kufanya kazi ya matanuri huku akiifanya kazi hiyo kwa kurithi kwa familia yake au sehemu nyingine ya jamii kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maisha yake ya kila siku. Picha na Kambi Mbwana.
0 comments

HIVI NDIO HALI YA JENGO LA WESTGATE BAADA LA SHAMBULIO LA AL-SHABAAB.

HIVI NDIO HALI YA JENGO LA WESTGATE BAADA LA SHAMBULIO LA AL-SHABAAB.

Picha za nje ya jengo la Westgate hazioneshi uhalisia wa hali iliyoko ndani ya jengo baada ya shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70.

a7
Picha hizi zinatoa picha halisi ya jinsi jengo hilo lilivyoharibika vibaya kwa ndani baada ya ghorofa tatu za jengo hilo kudondoka baada ya kupigwa mabomu katika mchakato wa kukabiliana na magaidi. 
a6
Picha hizi pia zinaonesha jinsi magari yaliokuwepo eneo la maegesho ya magari katika jengo hilo yakiwa yameharibiwa kiasi kwamba kuna mengine ambayo huenda hata wamiliki wanaweza kushindwa kuyatambua.
a1
a2
a3
a4
a5
a8
0 comments

Sheikh Sharrif Ahmed; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu..

Sheikh Sharrif Ahmed; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu..

shehki_871e3.jpg
Ni Rais wa Somalia. Kwa hakika, kwa sasa ndiye Rais wa nchi ya Kiafrika mwenye wakati mgumu sana. Na katika shida zake, Sheikh Sharrif ameonekana, si mara moja, akitua Dar Es Salaam, kwenye Ikulu ya JK. Kwa Sheikh Sharrif aliye matatizoni, kufunga safari ya Dar kwa JK ni kama kwenda kwa Obama! Kuna tofauti kubwa na Mogadishu.
Kiukweli Sheikh Sharrif Ahmed hana eneo kubwa la nchi ambalo anaweza kusema kuwa analidhibiti. Kuna wakati ikasemwa, kuwa anadhibiti maeneo jirani tu na Ikulu yake ya Mogadishu. Huko kwengine kuna ' Mabwana wa Vita'.
Na sasa ni ' pasua' kichwa ya Al shabaab. Tofauti na inavyoonekana nje, Al shaabab hawajawa na nguvu za kutisha sana. Isipokuwa, wakiachwa wakue, ni ' pasua' kichwa si tu kwa Somalia, bali kwa nchi zetu hizi.

Shambulizi la Wastgate ni ishara za Al Shabaab wanaoanza kuota mapembe. Kuna mantiki ya Marais wa nchi jirani na Somalia ikiwamo Tanzania, chini ya mwevuli wa AU na UN, kufanya jitihada za kuungana katika kupanga mikakati ya kumsaidia Sheikh Sharrif Ahmed.
Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab, ambayo kimsingi, haina sapoti ya Wasomalia wengi.
Wikiendi Njema.
Maggid.

0 comments

Nawashukuru kwa kuniombea:Awila Silla

Nawashukuru kwa kuniombea:Awila Silla

20130923_113144_187fa.png
20130923_113248_89d98.png
Mlinipenda, mkanijali na kunithamini sana katika taabu na mateso makali ya mapanga siku 17 zilizopita. Namshukuru kila mmoja aliyetaabika na kuamua kuteseka kwa sala kwa ajili yangu na katika kila hali, hakika Mungu amependezwa na kusikia. Mungu ni mwema naendelea vyema kama mnavyoniona. Sina cha kuwalipa Mungu awaone katika kila hitaji na hatua za maisha yenu.Na Awila Silla 


0 comments

meza ya magazeti leo jumamosi

0 comments

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MIZENGO PINDA ALIVYOZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI KTK HOTELI YA MKONGE JIJINI TANGA.

WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MIZENGO PINDA ALIVYOZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI KTK HOTELI YA MKONGE JIJINI TANGA.

WAZIRI MKUU MH, MIZENGO PINDA AKITOKA NJE YA UKUMBI WA HOTELI YA MKONGE BAADA YA KUTOA HOTUBA KTK UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI.

MKUU WA WILAYA YA HANDENI MH, MUHINGO RWEYIMAMU ALIYEVAA SUTI NYEUSI AKITOA MAELEKEZO KWA MMOJA WA RAIA AMBAYE AKUFAHAMIKA UTAIFA WAKE KUHUSU FULSA ZA UWEKEZAJI ZINAZOPATIKANA KTK WILAYA YA HANDENI


0 comments

MAPOKEZI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA MKOANI TANGA.

MAPOKEZI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA MKOANI TANGA.


Mhe. Peter Kayanza Pinda , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika Mkoa wa Tanga kwa ajili ya Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini litakalofanyika Septemba 26-27 mwaka huu. Mara baada ya Mapokezi Mhe. Pinda atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Tanga katika ukumbi wa mikutano wa Tanga Beach resort.

 Mhe.  Pinda akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa

3 &4 Mhe. Pinda  akisalimiana na Viongozi wa ngazi za juu katika Mkoa wa Tanga.



.Mhe. Mizengo Pinda akifurahia burudani ya vikundi mbalimbali ( havipo pichani) mara tu baada ya kuwasili katika Mkoa wa Tanga. ( wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Ndedego na kulia kwake ni Mama Pinda , mke wa Waziri Mkuu Mhe . Pinda.

6&7. Burudani mbalimbali. Picha zote na Monica Laurent, Afisa Habari Mkoa wa Tanga.

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger