Mshambuliaji
wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa (katikati) akiwa ameshika risiti ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kulipa Sh. Milioni 45,
alizotakiwa kuilipia klabu ya Simba SC. Wengine kulia ni Ofisa Habari wa
Yanga SC, Baraka Kizuguto na kushoto Mhasibu, Rose Msamila. Ngassa
alifungiwa mechi sita za mashindano na TFF pamoja na kutakiwa kurejesha
fedha za Simba Sh. Milioni 30 na fidia ya Sh. Milioni 15, baada ya
kubainika alisaini timu mbili, Simba na Yanga alikoidhinishwa kuchezea
msimu huu.
|
Post a Comment