Sheikh Sharrif Ahmed; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu..
Kiukweli Sheikh Sharrif Ahmed hana eneo kubwa la nchi ambalo anaweza kusema kuwa analidhibiti. Kuna wakati ikasemwa, kuwa anadhibiti maeneo jirani tu na Ikulu yake ya Mogadishu. Huko kwengine kuna ' Mabwana wa Vita'.
Na sasa ni ' pasua' kichwa ya Al shabaab. Tofauti na inavyoonekana nje, Al shaabab hawajawa na nguvu za kutisha sana. Isipokuwa, wakiachwa wakue, ni ' pasua' kichwa si tu kwa Somalia, bali kwa nchi zetu hizi.
Shambulizi la Wastgate ni ishara za Al
Shabaab wanaoanza kuota mapembe. Kuna mantiki ya Marais wa nchi jirani
na Somalia ikiwamo Tanzania, chini ya mwevuli wa AU na UN, kufanya
jitihada za kuungana katika kupanga mikakati ya kumsaidia Sheikh Sharrif
Ahmed.
Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab, ambayo kimsingi, haina sapoti ya Wasomalia wengi.
Wikiendi Njema.
Maggid.
Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab, ambayo kimsingi, haina sapoti ya Wasomalia wengi.
Wikiendi Njema.
Maggid.
Post a Comment