BABU WA LOLIONDO ATABIRI"HIVI KARIBUNI TANZANIA ITAKUWA KIOO CHA AFRIKA NA DUNIA"

BABU WA LOLIONDO ATABIRI"HIVI KARIBUNI TANZANIA ITAKUWA KIOO CHA AFRIKA NA DUNIA"

 
MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapila ‘Babu wa Loliondo’ amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na baadaye kioo cha dunia.

 Ametoa kauli hiyo Septemba 24, mwaka huu mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha. 

Mchungaji Mstaafu Mwaisapila aliyesifika kwa tiba ya kikombe cha dawa, alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia na hayakutokea Israeli sasa yatafanyika Samunge. “Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nimeyaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa. 

Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameonyeshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa ‘kugawa kikombe’ ikiwemo mahema, maji na ulinzi. Pamoja na maono hayo aliyopewa Babu wa Loliondo, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT), marehemu Moses Kulola alikuwa akimpiga waziwazi katika mahubiri yake akidai mwenendo wa tiba alizokuwa akizitoa hazifanani na mafundisho ya Mungu. 

Kama hiyo haitoshi, watumishi mbalimbali wa Mungu wamekuwa hawamuamini. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ kwa nyakati tofauti waliwahi kunukuliwa wakisema hawana imani na tiba ya kikombe iliyokuwa ikitolewa na Babu wa Loliondo



Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger