·
BWAWA LA MAJI MABAYANI AMBALO NDILO LINALOTEGEMEWA NA WAKAZI WA JIJI LA TANGA.
Mamlaka ya maji safi na maji
taka mkoa wa Tanga, Tanga UWASA inatarajia kuongeza mitandao ya usambazaji wa
maji ktk baadhi ya maeneo ya jiji la Tanga, kwa lengo la kuboresha huduma ya
upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa maeneo ya pembezoni mwa jiji
la Tanga.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni kwenye
hafla ya kusimika bodi mpya ya mamlaka hiyo iliyofanyika hivi karibuni mkoani
hapa na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na Serekali.
Maeneo yatakayonufaika kutokana na
kuboreshwa kwa mitandao hiyo ya maji safi ni pamoja na Kange masiwani, Kange
Mkurumuzi, Mwakidila C na baadhi ya maeneo ya mji wa Pongwe.
Kwa upande wa maji taka mamlaka imekwisha
tenga fedha kwa ajili ya upanuzi ambao hadi sasa bomba la maji taka la barabara
ya tano upo ktk hatua ya mwisho na pia ulazaji wa mabomba maeneo ya barabara ya
Mnyanjani Lumumba kwa barabara ya 13 utafanyika mwaka huu wa fedha.
Mbali na maboresho hayo mamlaka hiyo pia
inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji kupitia mpango wa maendeleo ya
sekta ya maji ktk maeneo ya pembezoni mwa mji ambapo inatarajiwa ifikapo mwaka
2015, wakazi wote wa pembezoni mwa jiji la Tanga watakuwa wanapata maji safi na
salama.
Post a Comment