MKUU wa mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa,
amemuweka rumande Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Najim
Mpate, kwa madai ya kumdharau wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Tukio hilo lilitokea jana wakati Mpate
alipokuwa anatoa maelezo kufuatia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali kwa Halmashauri ya Pangani ambapo ilionek
ana kuna hoja ambazo
hazijapatiwa majibu tangu mwaka wa fedha 2008/2009.
Hoja kuu inayoongelewa ni ile inayohusu
mkandarasi mmoja aliyelipwa fedha zaidi ya mkataba ulivyokuwa unaonyesha hivyo
Mkuu wa Mkoa alikuwa anataka maelezo kwa nini hoja hiyo ya karibu miaka mitano
iliyopita inaendelea kujirudia na kwanini mkandarasi husika hajarudisha fedha
hizo ili kufuta hoja hiyo.
Mara baada ya kujieleza Mkaguzi huyo alilipiga
chini kabrasha alilokuwa amelishinda, kitendo ambacho kiliwashtua madiwani
kwani kilionekana kuwa ni dharau ya wazi kwa Mkuu wa Mkoa.
Bada ya tukio hilo, hilo Mheshimiwa Gallawa
alisikika akisema, “Hivi huyu ni nani mbona amekaa kijeuri. Kwanza unajibu
maswali kijeuri, lakini mimi ni mtu wa kunitupia faili chini” Hii ni
halmashauri yako? OCD mchukue huyu mtu ukampumzishe.”
Akieleza baada ya kuisha kikao, Mheshimiwa
Gallawa alisema yeye ndiye anawajibika HAlmashauri zinapokuwa na hoja
zilizokosa majibu na hivyo hatakubali wazembe wachahce kwenye halmashauri
wamharibie dhamana aliyopewa ya kuwatumikia wananchi.”
Chanzo Juma Mtanda.blogspo.com
Post a Comment