UKATILI:! JAMAA MMOJA MKAAZI WA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA AMUUA MKEWE! SOMA KISA HAPA
Na Steven Augustino wa Demashonews Namtumbo,
Mfugaji wa Jamii ya Kisukuma anayeishi katika Kijiji cha Mtelamwahi Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina la Maiko Sajini(24) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumuua Mkewake kutokana na kilicho daiwa kuwa chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa kimapenzi.
Shuhuda wa tukio hilo Anna Yohana ambaye ni mjomba wa
Marehemu alisema kuwa Marehemu Dagwanedi Jogi (22) alikubwa na makasa huo baada ya mumewe huyo kumtuhumu kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja Kijijini hapo hali ambayo ilizusha mtafaruku huo kati ya wanandoa
hao. Alisema siku ya tukio mumewe huyo alisafiri kwenda kijiji jirani nakwa kawaida yake huwa anarudi usiku wa manane kama alivyo fanya siku hiyo,lakini kila anapo rudi humkuta mkewe akiwa amelala lakini cha kushangaza wakati akikaribia nyumbani hapo alikutana na kijana huyo njiani ambaye kila mara alidai kuwa amekuwa akimhisi kumuiingilia katika ndoa yake na hata alipofika nyumbani kwake alimkuta mkewe akiwa hajalala hali ambayo ilimfanya amhoji juu ya hali hiyo.
Alisema wakiwa katika mahojiano hayo ilitokea kuto elewana kati yao ambapo mwanaume huyo aliomba amkague mkewe huyo katika sehemu zake za siri ili kujiridhisha juu ya mashaka yake hayo lakini marehemu
alikataa kata kata hali ambayo ilimfanya mtuhumiwa huyo kutumia nguvu katika ukaguzi huo ambapo baada ya kuangalia aligundua kuwa mkewe huyo alikuwa ametoka kufanya tendo hilo alilo lihisi.
Akizungumzia tukio hilo mtendaji wa kata ya Ligera Alli Manoni alisema kuwa baada ya kupokea taarifa hizo yeye kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji cha Mtelemwahi walienda eneo la tukio na kushuhudia unyama huo lakini kwavile mtuhumiwa alikuwa amekimbia walitoa taarifa Polisi ambao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa anaelekea katika Kijiji cha Suruti Wilaya ni humo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusidedith Nsimeki amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za mauaji hayo baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi.
Aidha Kamanda Nsimeki aliendelea kufafanua kuwa pamoja na mambo mengine Polisi wanaendelea kumsaka mtu ambaye alidai kuwa chanzo cha ugomvi huo ambao ulisababisha mauaji hayo ambayo hadi sasa jina lake halijafahamika.
Post a Comment