Rais mpya
wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)
iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
TanzaniaSheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika
sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National
Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish
Rais mpya
wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
TanzaniaSheria Ngowi akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia katika
sherehe za zilizofanyika jana asubuhi katika viwanja vya National
Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish.
Rais mpya
wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)
iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
TanzaniaSheria Ngowi akipokea salaam Maalum Kutoka kwa Rais wa Mpito wa
ZambiaGuy Scotts Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za
kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini
Lusaka-Zambia.
Rais mpya
wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential
suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini
Tanzania Sheria Ngowi akiwa na Mkewe Eshter Lungu Muda mfupi baada ya
kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja
vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
-----
Mbunifu
wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya
Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana
asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
Rais
Lungu 58, aling'arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi
(Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu
zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu
aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani
hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.
Akizungumza
baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya
kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na
kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa
kimataifa.
"Hii ni
hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa
kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike
hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya
wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu", alisema Ngowi.
Mbunifu
Ngowi alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele
ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na
malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata
kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na mke
wake Charlotte, Mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za
kusini(SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu
wa Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi wake.
Mbunifu
huyo ameendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye
vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake
katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata
mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri
kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika
maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani
na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.
Hii ni
changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia
kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la
kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua mlango.
VICTOR SIMON