HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAOMBWA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA KUNUNULIA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU.

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAOMBWA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA KUNUNULIA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU.

SHIRIKISHO la Vyama watu wenye Ulemavu mkoani Tanga (Shivyawata) limeiomba Halmashauri ya Jiji la Tanga kuangalia uwezekano kuwatengea bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa visaidizi kwa jamii hiyo.

Vifaa hivyo ni pamoja na fimbo nyeupe, kiti mwendo (wheelchair) Shime Sikio,(hearing aid) na Mashine ya kuchapia ambapo bila kutegemea msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na Halmashauri hawawezi kuvipata.

Ombi hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Zuhura Mussa wakati alipokuwa akizungumza na Mtandao huu ambapo alisema kuwa jamii hiyo imekuwa ikikumbana na changamoto hiyo kutokana na kuwa vifaa hivyo ni ghali hivyo familia nyingi hushindwa kumudu gharama
zake.

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo lakini wanaiomba
Halmashauri hiyo kuhakikisha miundombinu iliyopo chini yake inakuwa rafiki kwa jamii hiyo pamoja na kuwapa kipaumbele kwenye masuala ya afya katika vituo vya afya na zahanati.

   “Changamoto zinazoikabili jamii ya watu wenye ulemavu ni nyingi lakini hili la vifaa kwetu ni kubwa hivyo tunaiomba Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo mkoani hapa kuangalia uwezekano wa kutusaidia “Alisema Zuhura.

Alisema kuwa changamoto nyengine ambazo wanakumbana nazo ni kutokuwepo kwa wataalamu wa kutosha katika mashule kwa ajili ya kusaidia na kufundisha watoto wenye ulemavu au kugundua ulemavu wao mapema.

Hata hivyo aliongeza kuwa ufinyu wa bajeti ya kuendesha shughuli zao za kila siku huwalazimu viongozi kufanya kazi za kujitolea na wakati mwengine kushindwa kufikia malengo yao kutokana na uhitaji wa fedha jambo ambalo linachangiwa kwa asilimia kubwa na kukosekana kwa wafadhili na fungu maalumu kutoka halmashauri
.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger