Equatorial Guinea na Congo zasonga mbele
Wenyeji
Equitoria Guinea na Congo Brazaville zimekuwa timu za kwanza kusonga
mbele katika hatua ya robo fainali kutoka kundi A ya Michuano ya Fainali
ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada timu hizo shindi mechi zao hapo
jana usiku.
Equitoria
Guinea iliwaadhibu wapinzani wao Gabon kwa jumla ya magoli 2 bila
majibu, huku Congo Brazaville nayo ikiwashushia kipigo Burkina Faso cha
magoli mawili kwa moja.
Wenyeji
Equitorial Guinea waliandika bao la kwanza katika dakika ya 55 kipindi
cha pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Lloyd Palun kufanyiwa faulo
katika eneo la hatari.
Kama hiyo
hatoshi Wenyeji hao wakapigilia msumari wa moto kwenye kidonda pale
waliondika bao la pili kupitia Salvador Iban ambaye aliukwamisha mpira
wavuni uliotemwa na mlinda mlango wa Gabon.
Nayo
Congo Brazavile ambayo ilihitaji sare ya aina yoyote ili isonge
mbelehatua ya robo fainali ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa
mchezaji Thierry Bifouma huku goli la pili likifungwa na Fabrice Ondama.
Goli pekee la Burkina Faso lilitiwa wavuni na Aristide Bance.
Kwa
matokeo hayo Congo Brazaville inaingia hatua ya robo fainali kwa mara ya
kwanza ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa mara kwanza tangu
mwaka 1992.
Leo
kutakuwa na mechi mbili za kundi B ambapo timu mbili kutoka ukanda wa
Afrika Mashariki na kati Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia
zitatupa karata zao za mwisho ambapo Jamuhuri Kidemokrasia ya Kongo
itaumana vikali na Tunisia huku Zambia ikikutana uso kwa uso na Cape
Verde.
Zambia na
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lazima zishinde mechi zao leo ili
ziweze kusonga mbele hatua robo fainali huku Zambia ikihitaji ushindi wa
magoli zaidi ya matatu kwa bila.
Post a Comment