SOKO LA SAMAKI, DEEP SEA KAMA LINAVYOONEKA IJUMAA YA LEO
Eneo maarufu jirani na bandari ya Tanga inayojulikana kwa jina la deep sea, eneo ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa samaki wa aina mbalimbali, nalo ni miongoni mwa maeneo yaliyokumbwa na chungu ya msalagambo
Masalia ya vifaa vilivyokuwa vimetumika ktk ujenzi wa mabanda ya biashara ktk eneo hilo la deep sea
Ni zaidi ya
miaka miwili au mitatu mpaka sasa halmashauri ya jiji la
tanga linatekeleza na kuendeleza kampeni ya weka jiji katika hali ya
usafi ambayo inatambulika na kila mmoja wa wakazi wa jiji la Tanga kwa kushiriki
kufanya usafi katika mazingira wanayoishi na pia kujitoa kikamilifu kufanikisha zoezi hilo lifanikiwe
Viongozi wa
ngazi ya mkoa,wilaya,tarafa, kata kijiji hadi mtaa wameweka utaratibu
wakuwafanya kila mmoja aweze kushiriki kikamilifu kutekeleza kampeni ya kuweka
jiji katika haliya usafi ambayo imepewa jina la kalembo day abayo wakazi
wanashiriki kwa pamoja kusafisha na kuzibua mitaro au kurekebisha sehemu kolofi
ndani ya maeneo yao,
yote kufanikisha kampeni hiyo.
Je,unajua
kwanini kampeni hiyo imepewa jina la kalembo daya.imetokana na jina la
aliyekuwa mkuu wa mkoa wa tanga said said kalembo alivyo shikiria kidete na
kusimamia zoezi hilo kwani ilimlazimu kupita mitaani na kuamasisha usafi wa
mazingira lifanikiwe, kwa upande mwengine zoezi hilo lilionekana kama na la watu
wachache au ubabe binafsi kwa viongozi
tu,kumbe siyo sahii bali hiyo ni
la wote nakuweka afya ya wananchi kuwa bora.
Utaratibu
uluwekwa kila jumamosi yakwanza ya mwezi zoezi hilo linafanyika kwa kila mmoja
pia ililazimika kutolewe amri kila mfanya biashara mkubwa au mdogo kuto fungua
biashara yake mpaka saa tatu asubihi, hali hiyo ilifanyika kila mwezi kwa
umuhimu wajambo hilo viongozi waka onelea iendelee kwa kila wiki ili kuendeleza
na kutekeleza zoezi hilo na limepiga hatua na mafanikio yanaonekana.
Baada ya
kuondoka mkuu wa mkoa huyo utawala ulishikwa na luteni mstaafu bi chiku galawa
ambaye amesima kidete kuendelea na kutekeleza kwa vikali swala hilo kwa kutoa mwanya kwa taasiai
binafsi,mashirika,vyama vya siasa,vikundi mbalimbali,vyombo vya habari na mtu mmoja mmoja kwanafasi yake kufanikisha
kampeni ya msalagambi(kalembo day) cha kupendeza zaidi
wasani wa
vikuni vya ngoma,maigizo na wale wa kizazi kipya wametumia vipajivya kwa
kutunga na kuimba amakuigiza ili kufikisha ujumbe wa kufanya usafi wa jiji la Tanga.
Ila ukitaka
maendeleo na afya bora nilazima maeneo yaani mazingira tunayoishi yawe masafi
itafayanya kuimarisha upana wa mawazo wakufikiri na magonjwa yanayo sababishwa
na uchafu yatapungua,kwani kwasasa jiji la tanga nitofauti na kipindi cha nyuma
magonjwa kama kipindu pindu na magojwa mengine yanayo sabaisha yamepungua wa
mujibu wa wakazi wa jiji hili
Kwa sasa
hali ya usafi kwa jiji la tanga linavutia na kulizisha kwani wahenga walisema
mwenye macho ambiwi tazama pia wakazi wa jiji hilo wanatama wageni siku baada
siku na kwapamba kwa ule usemi wao usemao “waja leo waondoa leo” huu usemi
unamaana kubwa sana hatakama ulikuja wawenyeji hao na kuaa mwezi wao wanaona ni
muda mfupi basi wanazidi kuwapoke wageni mbalimbali baada ya kampeni hizo
ambazo zina endele mpaka na mafanikio yanaoneka.
Hata hivyo
hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Tanga Chiku Galawa alipokuwa akifungua mafunzo
ya watafiti wa kutambua watu wenye uwezo wa kufanya kaziuliyo fanyika jiji hapa
wa kanda ya masariki yaani Arusha,Kilimanjaro,manyara na tanga alitumia nafasi
hiyo kuwakaribisha wageni hao kwakusema “jiji la tanga ni safi,mazingira mazury
bustani za mapumziko na sehemu za burudani zipo za tosha muwe na amani karibuni
tanga mkatangaze uzuri wetu”
Kwa pamoja
tunaweza endapo tukishirikiana kwa pamoja kwani changamo ndani ya zoezi hilo zipo ila tujivunie
matokeo tuliyo yapata tusiishie hapa tuwaunge mkono viongozi tunaweza. Vizuri
vina higwa tuige mfano wajiji la tanga kwa kampeni yao ya kalembo day.
Post a Comment