ANATAFUTWA NA POLISI TANGA KWA KUMUUA MWENZAKE KTK UGOMVI WA WA KUGOMBEA SIGARA.
Jeshi la polisi mkoa wa Tanga linamsaka mtu mmoja
baada ya kumuuwa mwenzake wakiwa wanagombania sigara.
kamanda wa polisi
mkoa wa Tanga Costantino Masawe (pichani)amemtaja
mtu huyo ambaye amefanya tukio hilo kuwa ni Iddi mkono mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa kijiji cha
kwamdolwa kata ya kwamdolwa wilayani Korogwe mkoani hapa ambaye alimkata
mwenzake mkono kwa kutumia panga wakiwa wakigombania sigara na kumsababishia umauti.
Kamanda masawe amemtaja mtu aliyefariki kwa jina la
Ramadhani Budalo 35 naye anaishi katika
kijiji cha kwamdolwa kata ya kwamdolwa wilayani Korogwe mkoani hapa,
Hata hivyo watu hawa walikuwa katika ugovi na kufikia
atua ya kushikiana panga na mmoja akamuwahi mwenzie na kusababishia jeraha na
ikawa ndiyo mwisho wake na aliye fanya unyama huo alitoroka ambapo jitihada za
kumtafuta zinaendelea iliafikishwe kwenye vyombo vya sheria
Pia kamanda huyo akusita kutoa wito kwa wakazi wa mkoa
wa tanga kujiepusha na ugovi,kutofanya maamuzi ya gafra na kujichukulia sheria
mkononi kwani ni kofa pia inahatarisha amani ndani ya jamii.
Post a Comment