Mashindano ya Ngalawa yafana Tanga

Mashindano ya Ngalawa yafana Tanga

 

 Ngalawa zikiwa katika mstari kwa ajili ya kuanza mashindano katika pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.

Na Mwandishi Wetu, Muheza
Mashindano ya ngalawa yaliyofanyika jana Wilayani Muheza katika Kijiji cha Kigombe yamefana huku Kampuni ya simu ya ZANTEL  ikifanikisha kwa kutoa zawadi .

Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo amewataka vijana washiriki katika michezo badala ya kukaa vijiweni.
 
Kauli hiyo aliitoja wakati  akifungua mashindano ya kwanza ya Ngalawa mkoani Tanga yaliyofanyika kwenye Pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.

 Mwidau alisema kupitia michezo vijana wataweza kupata fursa nyingi ikiwemo elimu na ujunzi kutoka kwa wenzao ,burudani pamoja na kujenga afya za kimwili na kiakili.

 “Mahindano haya ya Ngalawa hapo awali yalikuwa yanafanyika ngazi ya kijiji lakini kupitia kwa wadhamini Kampuni ya simu ya ZANTEL tumeweza kuyafanya kimkoa kwa lengo la kuibua fursa za ajira kwa vijana na kwashirikisha watu katika michezo, ”alisema Mwidau.

 Nae Meneja mauzo wa  ZANTELTanzania  Salum Ngururu,  alisema kuwa  lengo la kudhamini mashindano hayo ni kurudisha faida wanayopata kwa jamii kutoka na huduma zake na kuendelea kuwatambulisha bidhaa zinazotolewa na kampuni hiyo.

Alisema ZANTEL itakuwa ikiboresha zawadi za mashindano hayo kila mwaka ili yaweze kuvuta washiriki wengi.

Mshindi wa kwanza alijipatia kitita cha Shilingi laki tatu, kikombe cha ushindi pamoja na medali za dhahabu. Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka ambaye aliweza kujinyakuliwa zawadi hiyo.

Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya Ngalawa thelathini zilizokuwa na washiriki watano ambapo washiriki walitoka katika Wilaya za Tanga, Pangani na Muheza huku Wilaya ya Mkinga ikishindwa kushiriki kutokana na kushindwa kufanya maandalizi mazuri.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger