WAGOSI WA KAYA WAANZA RASMI KAMBI YA MAZOEZI OMANI

WAGOSI WA KAYA WAANZA RASMI KAMBI YA MAZOEZI OMANI 






















TIMU ya Coastal Union jana iliwasili jijini Muscat Oman usiku saa sita na kufikia katika hoteli ya City Centre.
Kaimu balozi wa Tanzania nchini Oman, ndie alietupokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mascut na kutuelekeza vema kuhusu masual mazima ya mji huo.
Nae mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Talib Hilal alikuja hotelini na kuzungumza nasi juu ya masuala mazima ya soka nchini hapa.
Talib, ndie mwenyeji wetu ambae anaratibu kila tukio tutakalofanya kuhusu mechi na mazoezi ya timu. Vilevile atahakikisha maisha yetu mjini Mascut yanakuwa rahisi kwa kusimamia masuala ya usafiri na mambo yote muhimu.
Kesho saa tisa alasiri timu itashuka dimbani katika uwanja wa Musanaa ambapo tutacheza mechi ya kirafiki na timu ya Musanaa ambayo ipo ‘top four’ ya ligi kuu ya Oman.
Aidha zipo taarifa zilizotolewa na moja ya gazeti la udaku juu ya hali mbaya ya maisha kwa timu ya Coastal Union, nchini Oman. Lakini nadhani picha zinazungumza maneno mengi kuliko maandishi. Hivyo kwa nafasi ya usemaji nahakikisha kuwa vijana wapo katika hali nzuri na hakuna matatizo yoyote.
Kwa mujibu wa mkuu wa msafara ambae pia ni mwenyekiti wa Wagosi, Hemed Hilal ‘Aurora’ timu itacheza mechi nne za majaribio kabla ya kurudi Tanzania baada ya wiki mbili.
Taarifa nyingine zitaendelea kutolewa kupitia vyanzo vyote vya Coastal Union……
COASTAL UNION
MUSCAT, OMAN
10 JANUARI, 2014
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger