UVUNAJI WA MAZAO YA BAHARI UMEPUNGUA KUTOKA TANI 481 HADI TANI 316 MKOANI TANGA
Tanga.
HALI ya uvunaji wa mazao
ya baharini katika mkoa wa Tanga imepungua kutoka tani 481 zilizopatikana mwaka
2011/2012 zenye thamani ya fedha za kitanzania 4,821,440,915.15
zilizosafirishwa nje ya nchini hadi kufikia tani 316 kwa mwaka 2012/2013 ambapo
upungufu huo wa tani 165.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku
Gallawa wakati akizungumza na TANGA RAHA BLOG ambapo alisema upungufu huo
umesababishwa na hali ya soko la mazao kama Pweza kwa nchi Ulaya kupungua.
Gallawa alisema sekta ya uvuvi mkoani Tanga imeendelea
kutunza mazingira ya uzalishaji wa mazao ya majini kwa kudhiti uvuvi haramu ambapo mwaka 2011-2012 jumla ya doria 120
zilifanyika na kufanikiwa kuwakamata
wahalifu 20 na kuwafikisha mahakamani.
Licha ya kuwakamata watuhumiwa hao pia walikamata vyombo vya
baruti 6 na baruti 10 na bunduki 5 za
kuvulia zilikamatwa,Samaki wa baruti kilo 240 walikamatwa na kutekelezwa na
makokoro ikiwemo juya 60 ambavyo
vilikuwa vikitumika kwenye uvuvi haramu.
Aidha alisema jumla ya kesi 22 zilifuatiliwa mahakamani
ambapo kesi CC 06/2009 inayohusu mtu mmoja kwa kosa la kupatikana na samaki wa
baruti ilitolewa hukumu ya kifungo cha miezi mitatu jela na kesi CC 363/09
inayohusu mtu mmoja kupatikana na samaki w baruti iliyotolewa hukumu ya
kumuachia huru mshtakiwa wakati kesi
nyengine zilikuwa zikiendelea.
Mkuu huyo wa mkoa alisema katika kipindi cha mwaka 2012-2013
Jumla ya doria 44 zilifanyika na kesi 10 zilifuatiliwa mahakamani ambapo jumla
ya vyombo vya baruti 20 vilikamatwa pamoja na sanmaki wa baruti 160
walikamatwa.
Post a Comment