Hii ni kutoka Kenya jamaa amefufuka akiwa chumba cha kuhifadhia mait
Hii
ni kutoka kwa majirani zetu ambapo tunaambiwa Wananchi wa Kenya
wameshangazwa na taarifa ya mwanaume mmoja aliyedhaniwa kuwa amekufa na
kufufuka akiwa chumba cha kuhifadhia
maiti katika hospitali moja mjini Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Jamaa
huyo anaitwa Paul Mburu ana umri wa miaka 24 ambapo alipelekwa
hospitalini kwa matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai
kutokana na ugomvi wa kifamilia na babake ingawa ilisemekana jamaa
alifariki Jumatano usiku wakati akipokea matibabu.
Wafanyakazi
wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na wengine kukimbia walipoona
mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki ukitembea na kuonyesha dalili za kuwa
hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Afisa
mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya Dokta Joseph Mburu
amesema kuwa dawa iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo kupiga polepole
hali ambayo huenda ilimfanya muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua
amefariki.
Raia
huyo wa Kenya alisikika akimtaka mmoja wa wafanyakazi katika chumba cha
kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na hapo
ndipo mmoja wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.
Ndugu
wa jamaa huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha
kuhifadhia maiti siku ya Alhamisi ili kuanza kwa taratibu za mazishi
lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.
Mgonjwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Naivasha.
Post a Comment