ANGALIA ERNIE BRANDTS ALIVYOONDOKA DAR KIMYAKIMYA
Kocha aliyetimuliwa Yanga, Ernie Brandts
amechukua uamuzi wa kuondoka nchini kimyakimya.
Brandts aliondoka nchini juzi usiku na
kuwasili nchini Uholanzi jana asubuhi.
Alipoulizwa sababu ya kuondoka
kimyakimya huku akiwa ametangaza ataondoka usiku, Brandts alisema anaamini wazo
lake lilikuwa zuri kiusalama.
“Sijui kwa nini nimekuwa na hofu, lakini
nimeona hivi ni sahihi.
“Nashukuru niko hapa uwanja wa ndege na
ninaondoka kurejea nyumbani.
“Mke na mtoto wangu wananihitaji na
ninaamini kipindi hiki ndiyo bora cha kurejea nyumbani na kuwa pamoja na
familia yangu,” alisema.
Brandts aliipa Yanga ubingwa na hadi
anafukuzwa, Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakifuatiwa na Azam
FC.
Alifukuzwa baada ya kikosi chake
kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya Bonanza la Nani Mtani Jembe
iliyopigwa Desemba 21, mwaka jana.
Post a Comment