DUNIANI KUNA MAMBO,TAMBUA MAMBO MANNE AMBAYOHUKUFAHAMU HAPO KABLA!!
1.Utafiti
uliofanywa barani ulaya umegundua kuwa wanafunzi ambao ni mashabiki wa
mchezo wa soka hufanya vibaya kwenye mitihani yao wakati timu zao
zinapofanya vizuri yaani timu inaposhinda takwimu za matokeo ya mitihani
huwa chini.
2.Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na The Happy Planet Index nchi inayoongoza
kwa furaha duniani ni Costa Rica,marekani inashika nafasi ya 105 kwenye
orodha ya nchi zenye furaha duniani.
3.Kuna
kitabu kimoja ambacho kinaitwa “what every man thinks about apart from
sex” yaani “kitu ambacho wanaume wanafikiria tofauti na ngono”. kitabu
hiki kimewahi kuweka rekodi ya mauzo ya juu , cha kushangaza kuhusu
kitabu hiki ni kwamba kina kurasa 200 ambazo hazijaandikwa kitu chochote
ndani yake.
4.Nchi
ya marekani ni nchi ambayo inaongoza kwa kuwa na sheria za ajabu ,
mojawapo ya sheria hizo ni sheria iliyowekwa na serikali ya jimbo la
North Carolina ambayo inasema kuwa ni hatia kuimba off key yaani ukiimba
nje ya zile key za muziki basi umefanya hatia na unaweza kutozwa faini
au kutumikia kifungo gerezani.
Post a Comment