PUMZIKA KWA AMANI MTANGAZAJI MAHIRI JULIUS NYAISANGA
R.I.P
kwa Mtangazaji legend ambae atakumbukwa na Watanzania wengi nikiwemo
Mimi D'JARO ARUNGU, ni legend ambae upekee wa sauti yake pamoja na
ubunifu wa vipindi alivyoviendesha vilimpa heshima na jina lake kukua
kila siku kutokana na kumbukumbu aliyokua anaicha kwa watu kila
anaposikika.
Julius Nyaisanga ambae alifariki
dunia October 20 2013 hospitalini Morogoro kutokana na maradhi ya Presha
na kisukari, ameagwa Dar es salaam October 22 2013 na kusafirishwa
kwenda kuzikwa kwao Mara.
Mpaka anafariki, Nyaisanga ambae
amewahi kufanya kazi na vituo vikubwa kama TBC Zamani Radio Tanzania na
ITV/Radio One alifariki akiwa na umri wa miaka 53 ambapo ofisi yake ya
mwisho kuifanyia kazi ilikua Abood TV/Radio Morogoro.
Post a Comment