SIMBA YAVAMIA TANGA KWA HASIRA, COASTAL UNION YAWATULIZA
BAADA
ya kutoka sare ya mabao 3-3 na Yanga, kikosi cha Simba kesho jioni
kitashuka katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kuvaana na Coastal
Union ya mjini humo.
Kikosi
cha Simba kiliwasili Tanga jana mchana tayari kwa mchezo huo
utakaochezwa kesho saa 10:00 jioni na tayari shamrashamra zimeshaanza
kutawala jiji la Tanga.
Ofisa
Habari wa Simba, Ezekile Kamwaga ameuambia mtandao huu kwamba, kikosi
cha Simba kiliwasili salama jana jijini Tanga tayari kwa mchezo huo wa
kesho na wachezaji Hnery Joseph, Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud
hawapo katika kikosi hicho.
“Timu
imefika salama Tanga tangu jana mchana na hali ya kikosi kizima ni
nzuri kinachosubiriwa sasa ni muda kufika ili tuweze kutazama pambano
hili safi na la kuvutia kwetu sote, kwani Coastal ni timu nzuri ambayo
ina wachezaji kadhaa ambao wamewahi kuwika na klabu mbalimbali za hapa
nchini.
“Sisi
kama Simba tunaamini tuna timu nzuri ambayo inaweza kupambana na timu
yoyote na kutwaa ubingwa hivyo wakazi wa Tanga na miji ya jirani
wajitokeze kwa wingi uwanjani kutazama pambano hili la kuvutia,” anasema
Kamwaga.
Naye
Mwenyekiti wa Coastal, Ahmed Aurora amesema kikosi cha timu yake
kimejiandaa vya kutosha na hakuna tatizo lolote linaloikabiri timu yake
kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba.
“Sisi
tupo vizuri kabisa tunaisubiri Simba kwa hamu kubwa kuweza kupambna nao
kwani tumejiandaa vizuri chini ya kocha wetu Joseph Lazaro ambaye
amejiunga nasi hivi karibuni akichukua nafasi ya Ahmed Morocco.
“Tuna
wachezaji wengi wazuri ambao wamewahi kutamba na timu kubwa za Simba,
Yanga na Azam, tunachohitaji sisi ni kufanya vizuri kwenye uwanja wetu
wa nyumbani,” anasema Aurora.
Wachezaji
wa Simba waliowahi kuichezea Simba ni Haruna Moshi ‘Boban’, Juma
Nyosso, Jerry Santo na Pius Kisambale ambaye pia amewahi kuichezea
Yanga. Wachezaji wa Yanga waliowahi kuichezea Yanga ni Razack Khalfan,
Atupele Green, Shaaban Kado na Kisambale.
Post a Comment