Na Oscar Assenga, Mkinga
CHAMA cha Wananchi CUF wilayani Mkinga kimeelezea mikakati
yake ya kufanya mikutano ya hadhara katika kata zote zilizopo wilayani humo
lengo likiwa kukiimarisha chama hicho pamoja na kujiandaa na uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 ili kuchukua kata zote.
Akizungumza hivi karibuni,Mwenyekiti wa Chama hicho,Mauya
Kileo amesema anaamini lengo lao litafanikiwa kutokana na kukabalika vilivyo na
wananchi maeneo mbalimbali wilayani humo kitendo ambacho kiliwawezesha chama
hicho kupata kata saba kati ya 21 zilizopo.
Kileo amezitaja kata ambazo zimechukuliwa na chama hicho
wilayani humo kuwa ni Mtimbwani, Kwale, Manza, Boma, Doda, Moa na Duga Sigaya na
kueleza mikakati yao ni kuongeza idadi ya kata kwenye uchaguzi huo mkuu kwani
hilo linawezekana kutokana na mshikamano walionao.
Aidha aliwataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuonyesha
mshikamano ili kuweza kufanikisha malengo yao ya siku moja kuongoza halmashauri
yaweze kufanikiwa.
Post a Comment