OKWI AJIUNGA NA URA KUSUBIRI HATMA YAKE KWA WAARABU - FIFA YAWAPA ETOILE MPAKA MWISHO MWA MWEZI HUU KUWALIPA MIL 480 SIMBA
STRAIKA
wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi amejiunga na URA ya Uganda ili
kujiweka fiti akisubiri hatma yake kwenye klabu ya Etoile du Sahel ya
Tunisia.
Okwi
amegoma kuichezea Etoile du Sahel mpaka itakapommalizia malipo yake ya
kusaini mkataba pamoja na kumlipa malimbikizo ya mishahara ya miezi
mitatu.
“Nimetulia
kwanza nione suala langu linaendaje na suluhisho ni nini. Ninataka sana
kurudi uwanjani kucheza soka la ushindani,” alisema Okwi.
“Ishu
ni kwamba hawajanimalizia pesa ya kusaini mkataba pamoja na mishahara
yangu ya miezi mitatu sasa,” alisema Okwi ambaye anaendelea kujinoa na
URA ingawa haruhusiwi kucheza mechi ya mashindano kwa sababu ana mkataba
wa miaka mitatu na Etoile du Sahel.
Wakala
wa mchezaji huyo amesema kwamba wanaendelea na mazungumzo na Etoile ili
kutatua suala la Okwi ingawa habari za ndani zinasema kwamba anafanya
mpango wa kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu moja ya Daraja la Kwanza
Ulaya.
Okwi
aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda na kucheza dhidi ya
Senegal wiki iliyopita katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia na
kushuhudia kikosi cha Kocha Sredojevic Milutin ‘Micho’ kikiambuliwa
kipigo cha bao 1-0.
Wakati
Okwi akiwa na malumbano hayo na klabu hiyo ya Tunisia, Simba ambayo
ilimuuza nayo inasubiri malipo ya Sh480 milioni kutoka kwa Etoile du
Sahel ambayo iliahidi kulipa fedha hizo kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetoa mpaka mwisho wa mwezi huu Simba iwe imelipwa.
SOURCE: MWANASPOTI
Post a Comment