COASTAL UNION KUUMANA NA BANDARI JUMAPILI MKWAKWANI

COASTAL UNION KUUMANA NA BANDARI JUMAPILI MKWAKWANI

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga ambaye imesheheni nyota wake Juma Said Nyosso na Haruna Moshi ‘Boban’, itashuka kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili kumenyana na Bandari ya Mombasa, Kenya katika mchezo wa kirafiki kudumisha ujirani mwema baina ya miji hiyo ya Pwani.

Akizngumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Mratibu wa Mechi hiyo George Wakuganda alisema maandaliiz yanaendelea vizuri ambapo timu zote hizo zitatumia mechi hiyo kwa ajili ya maandalizi yao mechi zao zinazowakabili.

Kama ilivyo Coastal, ni moja ya timu tishio katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, kadhalika na Bandari inasumbua katika Ligi Kuu ya Kenya msimu huu ikijivunia baadhi ya wachezaji wa Tanzania kama David Naftali, Meshack Abel, Thomas Maurice na Mohamed Banka.

Ligi mbalimbali Afrika zimesimama wikiendi hii kupisha mechi za kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil na baadhi ya klabu zinatumia fursa hiyo kwa mechi za kirafiki.

Kwa Coastal ni mchezo unaokuja baada ya kucheza mechi za Ligi Kuu ugenini, ikishinda 2-0 dhidi ya JKT Oljoro mjini Arusha na kutoa sare ya 1-1 na Yanga Dar es Salaam, tena ikisawazisha kwa penalti dakika ya 90.

Utakuwa mchezo mwafaka katika wakati mwafaka kwa kocha Hemed Morocco ili kuangalia mapungufu katika kikosi chake kabla ya Ligi Kuu kurejea wiki ijayo. Coastal msimu huu imesajili kikosi tishio haswa kikiundwa na mseto wa wachezaji kutoka Kenya na Uganda.

Kikosi cha Coastal 2013 kimesheheni wachezaji mahiri akiwemo Seleman Kassim Seleman, Philip Mugenzi Metusela, Jerry Salim Santo, Razak Juma Khalfan, Othman Omar Tamimu, Abdulla Othman Ali (mpya, Huru), Mohamed Sudi Athumani, Crispine Odula Wadenya (mpya, kutoka Bandari FC ya Kenya), Marcus Rafael Ndeheli (mpya kutoka JKT Oljoro FC), HusseinIssa, Haruna Mosh(mpya kutoka Simba SC), Uhuru Seleman (mpya kutoka Azam FC), Juma Said Nyoso (mpya kutoka Simba SC) na Pius Kisambale.

Wengine ni Shaaban Hassan Kado, Mbwana Hamis Bakari, Kenneth Abeid Masumbuko (mpya kutoka Polisi Morogoro), Daniel Reuben Lyanga, Said Seleman Lubawa (mpya, kutoka JKT Oljoro FC), Abdi Hassan Banda, Mohamed Miraji Mtindi, Mansoor Alawi Mansoor, Hamadi Juma Hamisi, Behewa Sembwana Behewa, Yusuph Ibrahim Chuma, Yayo Wasajja Fred
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger