UVCCM TANGA KUANZA ZIARA KESHO MKOANI TANGA.
JUMUIYA wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM) inatarajia kuanza ziara yake kesho kwa mkoa mzima wa Tanga kukutana na viongozi wa umoja huo ngazi za wilaya pamoja na kufanya mikutano ya hadhara.
Akizungumza leo na Blog hii,Mwenyekiti wa Umoja huo,Abdi Makange amesema ziara hiyo itakuwa na
lengo la kukutana na mabaraza ya umoja wa vijana kila wilaya ili kuwekeana mikakati mbalimbali ya kuufanya
umoja huo uzidi kuwa imara pamoja na kuwashukuru wajumbe wa umoja huo.
Amesema suala lengine watakalolifanya katika ziara
hiyo ni kuangalia uhai wa jumuiya hiyo kwenye wilaya hizo utakaoendena sambamba
na ufunguzi wa matawi ya umoja huo lengo likiwa ni kuuimarisha
Makange amesema ziara hiyo kwa kila wilaya zitakuwa zikihitimishwa na ufanyikaji wa mikutano ya hadhara ambapo wananchi wa wilaya husika watapata nafasi ya kupata sera makini za umoja huo ambazo zitakuwa zikitolewa na viongozi wake.
Post a Comment