MELI NDOGO YA MV MERCI 11 YA MIZIGO YAZAMA BAHARI YA HINDI KATIKA GATI LA KILWA MASOKO USIKU WA MANANE.
Meli hiyo ikiwa imezama majini katika gati la Kilwa Masoko safari moja kwa pamoja:Akiongea na Globu ya Jamii hii iliyofika katika eneo hilo, meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary, alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea songosongo na kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo Nahodha wa Meli hiyo Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliyekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa.
Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana. Chanzo. Jamii forum
Post a Comment