MREMBO ANUSURIKA KUBAKWA BAADA YA KUVAA KIVAZI NUSU UCHI NA KUPITA MTAANI
Hapo Akisaidiwa na Wasamaria Wema Baada ya Kupewa Khanga |
MREMBO wa haja ambaye jina halikupatikana amenusurika kubakwa na wanaume baada ya kuvaa kivazi kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maungo yake nyeti.
Tukio hilo lilijiri sehemu yenye mkusanyiko mkubwa, Kariakoo jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa kwenye ‘shopping’ kwa ajili ya sikukuu ijayo ya Krismasi.
Likiwa linarandaranda maeneo hayo, Ijumaa Wikienda lilinasa laivu tukio hilo ambapo mrembo huyo alivuliwa nguo hadharani na kuacha ‘vitu’ njenje vikishuhudiwa hata na watoto waliokuwa wakimzomea.
Wanaume hao waliokuwa wakiongezeka na kuanza kumshika sehemu nyeti, walisababisha dada huyo kuanza kutoka nduki ambapo alizama kwenye duka moja kisha akasitiriwa kwa khanga na mama mmoja msamaria mwema.
Alipotoka bado wanaume waliendelea kumzingira ambapo ilimlazimu kutoa shilingi elfu hamsini kisha kurukia kwenye ‘kenta’ iliyomuondoa eneo hilo na haikujulikana alikoelekea kwa sababu gari hilo lilichomoka mbio huku akiwa amekoma ubishi wa kutembea nusu utupu.
Post a Comment