Featured Post Today
print this page
Latest Post

Wabunge 15 matatani

Wabunge 15 matatani

thomas1 e4385
Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaanika wabunge 15, waliobainika kuchukua posho za safari bila kusafiri huku wengine wakikatisha safari zao.


Akizungumza katika mahojiano maalumu jana na mwandishi wa gazeti hili, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah, alisema tayari fedha hizo zimesharejeshwa kwa kukatwa kwenye mishahara yao.

Dk Kashililah alisema baadhi ya wabunge waliomba wasikatwe fedha hizo kwenye mishahara yao, badala yake wazirejeshe wao wenyewe.

Hata hivyo, Katibu huyo wa Bunge alisema wabunge hao walishindwa kusafiri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuwa na ugeni wa viongozi wa chama na matatizo ya kifamilia.

"Kwa mfano Komba (Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba) alishindwa kwenda kwa sababu ya kutembelewa na ziara ya Katibu wake wa Chama (Abdulrahman Kinana) muda wa safari ukamalizika hivyo akashindwa
kusafiri na taarifa zilikuwepo ofisini," alisema Dk Kashililah na kuongeza.


Akizungumzia safari ya Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Freeman Mbowe nchini Uingereza, Dk Kashililah alisema Bunge halina uwezo wa kumzuia mbunge yeyote kufanya shughuli zake safarini baada ya kumaliza jukumu lililompeleka.

Dk Kashililah alisema Mbowe alikamilisha ziara yake ya Bunge na kwamba baada ya hapo aliendelea na shughuli za chama chake nchini humo.

"Suala hili lilikuwa limebeba hisia za kisiasa, baada ya kusikika tu bungeni basi vyombo vya habari vikaanza kuwahukumu wabunge ni mafisadi bila hata kutafuta ufafanuzi kutoka wetu. Sisi taarifa hizo tulikuwa nazo kabla ya hata ya kuibuka bungeni, lakini lilivyotafsiriwa sikupenda," alisema Dk Kashililah.

Dk Kashililahb alisema, "Bunge lilikuwa limeratibu jumla ya safari mbalimbali zilizokuwa zimependekezwa na Kamati 16, lakini hazikufanikiwa kwenda zote kwa pamoja.

Alisema ziara zote za kamati huandaliwa kwa mujibu wa kanuni ya 117 ambayo inazipatia mamlaka Kamati hizo kuandaa ziara inazooana zina manufaa kwa ajili ya kuboresha utendaji wake. Chanzo: mwananchi
0 comments

Dk Ngasongwa: CCM inababaika

Dk Ngasongwa: CCM inababaika


ngasongwa1 9cf74

Ni kutokana na viongozi wake kusema hadharani bila ya kutumia vikao vya chama

Dar es Salaam. Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa na katika Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, Dk Juma Ngasongwa amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinababaika katika kutekeleza majukumu yake.

Vilevile, chama hicho kimekumbwa mgawanyiko kati ya watendaji wake na Serikali na kwamba taifa lina ombwe la uongozi.

Kutokana na hali hiyo, Dk Ngasongwa ambaye pia ni kada wa CCM amemshauri Rais Kikwete kuwa mkali katika kusimamia watendaji wake anaowateua ndani ya chama na Serikali yake na kufuatilia na kupima utekelezaji wa yanayokubaliwa .

Alikuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake mkoani Morogoro anakoendesha maisha yake kwa kilimo cha mpunga baada ya kustaafu.
Dk Ngasongwa alisema kuwa mgawanyiko huo kati ya watendaji wa Serikali na CCM, umeondoa umoja siyo tu katika vyombo hivyo, bali pia miongoni mwa wabunge wa chama hicho tawala.

Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kutokea mambo mengi ikiwamo matukio ya mawaziri kushinikizwa kujiuzulu kama ilivyotokea hivi karibuni na kwamba kwa Serikali ya Awamu ya Nne hali hiyo imekuwa ikijirudia.
"Chama tawala kinababaika sana, tena hata watendaji wa CCM, wanawasema vibaya mawaziri hadharani, wakati wote ni wateuliwa wa Rais (Jakaya Kikwete) na ndiye mwenyekiti wetu wa CCM. Hii inakigawa chama. CCM ina utaratibu wake, kwa nini wasiitwe wakahojiwa ndani ya chama, badala ya kutajana hadharani:
"Sielewi kwa nini CCM inababaika. Inachotakiwa ni kuwa na mshikamano kwa wabunge wake kukutana mara kwa mara na kujenga msimamo. Hii ni kazi ya mawaziri na wabunge pia," alisema Dk Ngasongwa na kuongeza:
"...Tatizo uongozi haufanyi kazi vizuri, ndani ya chama chetu kuna mgawanyiko mkubwa hata katika Serikali, mfano Mwanasheria Mkuu (AG) anaposema baadhi ya mawaziri hawamsikilizi, hii 'No' (hapana), lazima kanuni za uendeshaji wa Serikali zifuatwe, hii ni muhimu."
Alisema hali hiyo inaonekana hata kwenye Baraza la Mawaziri na kwamba mgawanyiko pia upo ndani ya Bunge kwa wapinzani.

"Lakini kugawanyika kwa upinzani ni afadhali kuliko CCM, kwani matokeo yake ni kupunguza imani ya watu kwa Serikali yao na chama tawala," alisema.

Akinukuu maneno ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dk Ngasongwa alisema: "Nyerere alisema, bila CCM madhubuti nchi itayumba na ndiyo yanayotokea sasa.

"Msingi wa yote yanayotokea ni ubinafsi, ubepari...; turudi kwenye Ilani ya chama, tuzungumze, tufikie mwafaka, siyo kutukanana hadharani. CCM itoe mwongozo siyo kugawa wananchi."
Ngasongwa aliyeshika nyadhifa mbalimbali za kisiasa katika CCM na Serikali ikiwamo ujumbe wa Kamati Kuu (CC), ubunge wa Ulanga Magharibi, Waziri wa Maliasili na Utalii na baadaye Waziri wa Mipango, Viwanda na Uwezeshaji, alifafanua kwamba kuna ombwe la uongozi katika chama tawala, upinzani, Serikali hata bungeni.

"Kuna ombwe la uongozi siyo tu kwa wapinzani, hata sisi chama tawala CCM, Serikali, hata bungeni pia kuna mchanganyiko na yanaonekana waziwazi. Tunaona Spika anavyodharauliwa na wabunge. Bunge linaonyesha picha ya hali halisi ya nchi yetu ilivyo,"alisema Dk Ngasongwa.
Alipotakiwa kuzungumzia zaidi
tukio la hivi karibuni la Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wanne walioshinikizwa kujiuzulu kutokana na Ripoti ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili, alieleza kuwa hajaisoma kwa undani ripoti hiyo, lakini inaonyesha kuwa utekelezaji wake ulikuwa mbaya.


Hata hivyo, alisema kuwa kamati hiyo ilitakiwa kuainisha makosa ya watendaji wa operesheni hiyo na kuwaacha mawaziri wajipime na kujiuzulu wenyewe.

Alisema kwamba hatua ya wabunge na kamati kushinikiza mawaziri hao wajiuzulu iliwachongea kwa Rais Kikwete aliyeamua kuwafukuza kazi kwa lugha ya kistaarabu, hali ambayo alielezea kuwa inaweza kujenga uhasama baina ya wabunge, kamati na mawaziri walioondolewa.

Hivi karibuni Rais Kikwete alitengua uteuzi wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamshi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi pia Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo baada ya wizara zao kutajwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyopoteza maisha ya watu, mifugo na vitendo vya ukatili kwa binadamu.

Kuhusu kubadilika kwa mawaziri, Dk Ngasongwa alieleza kuwa jambo hilo siyo baya, lakini akasema kwamba likifanyika mara kwa mara linadumaza wizara kwa kukosekana mwendelezo wa utendaji.
 
"...Ikitokea mara kwa mara inadumaza utendaji, hupati 'continuity' (mwendelezo mzuri), kwani mawaziri huhitaji kujifunza na utekelezaji huhitaji muda. Continuity ni muhimu kwa mawaziri, hata watendaji wengine," alisema.

Hii ni mara ya tatu kufanyika kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, likiwamo lililotokea baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu. Chanzo: Mwananchi
0 comments

JK kupokea Rasimu ya Katiba Mpya Jumatatu

JK kupokea Rasimu ya Katiba Mpya Jumatatu

 

Tume  ya Mabadiliko ya Katiba inatarajiwa kuwakabidhi Marais Jakaya Kikwete na Dk Mohamed Shein, rasimu ya katiba mpya.

Hafla ya makabidhiano hayo itafanyika Jumatatu, kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Tume, Assaa Rashid, ilisema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kuendelea kuwepo kwa tume hiyo, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki, alisema tume itakabidhi nyaraka hizo na itaendelea na kazi.

Alisema itavunjwa kwa mujibu wa sheria baada ya rasimu hiyo kufikishwa na kusomwa kwenye Bunge Maalum la Katiba.

Taarifa ya Rashid ilieleza kuwa hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wa kisiasa, taasisi na asasi mbalimbali zikiwamo za kidini na kiraia pamoja na wananchi.

Taarifa hiyo ilisema Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, anatarajia kuwakabidhi Marais, ripoti ya mchakato pamoja na rasimu ya katiba mpya.

Rasimu hiyo imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyoyawasilisha kwa tume kupitia njia mbalimbali zikiwamo mikutano ya hadhara, barua pepe, njia ya posta, tovuti (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania) na mabaraza ya katiba.

Mchakato wa kupata katiba mpya ulianza Julai, mwaka jana baada ya kuundwa kwa sheria ya kuanzisha tume ya mabadiliko ya katiba.

Kwa mujibu tangazo la Rais Kikwete kuhusu kuandikwa katiba mpya Tanzania inatarajia kuwa na katiba mpya ifikapo Aprili 2014, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Baada ya kuundwa tume hiyo ilipewa miezi 18 ya kutekeleza jukumu la kukusanya maoni, kuyachambua na kutayarisha rasimu ya awali ili ijadiliwe na wananchi na kuandaa toleo hilo linalokabidhiwa kwa maraisi wiki ijayo.

Baada ya kuzunguka Bara na Visiwani Tume ilikusanya maoni kuyachambua na kutoa rasimu mpya iliyutoka  Juni mwaka huu na kujadiliwa kwenye mabaraza ya katiba ili kuiboreshwa zaidi.

Miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa na rasimu ya awali ni kuwepo kwa serikali tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mapinduzi ya Zanzibar na Tanzania Bara.

Kadhalika ilizungumzia kuwepo kwa wagombea binafsi, kuondoa viti maalumu vya ubunge, kuweka ukomo wa ubunge na kuainisha mambo ya Muungano kuwa saba.

Bunge Maalumu
Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, baada ya kukabidhi rasimu hiyo ni kuitishwa Bunge Maalumu la Katiba.

Wajumbe wake wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wawakilishi kutoka Baraza la wawakilishi Zanzibar na wajumbe 166 watakaochaguliwa na kutoka asasi za kiraia, vyama vya siasa, taasisi za elimu ya juu, wafanyakazi, wakulima na makundi maalumu. 

Bunge hilo litaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni kama Spika ambaye atakuwa na makamu na makatibu. Viongozi hao watachaguliwa kwa misingi ya Bara na Visiwani.
0 comments

Handeni wazitamani Simba na Yanga kukipiga kwenye Uwanja wa Azimio wilayani kwao

Handeni wazitamani Simba na Yanga kukipiga kwenye Uwanja wa Azimio wilayani kwao


Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, mkoani Tanga, Thomas Mzinga, amesema kwamba Uwanja wao wa Azimio unastahili kukutanisha vigogo vya Simba na Yanga, katika michuano yoyote nchini
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, pichani.
  Akizungumza na Handen Kwetu Blog mapema wiki hii wilayani Handeni, Mzinga alisema kuwa hiyo ni kutokana na maandalizi na mwonekano wa uwanja wao wa michezo.

Alisema kuwa Uwanja wao ni mkubwa na unastahili kukutanisha timu kubwa na vigogo wa Tanzania Bara, vikiwapo Simba na Yanga.

“Tunajivunia kuwa na uwanja mzuri na muwajulishe huko kuwa wanapaswa waje wacheze huku katika mashindano yao mbalimbali.

“Tunaamini Uwanja huu pia ukikamilika kwa baadhi ya ukarabati wake, basi utachangia kwa kiasi kikubwa kuleta watu mbalimbali, hasa timu kubwa zitakapokuja,” alisema Mzinga.

Hata hivyo, kiu ya Mzinga na viongozi wa serikali wilayani humo inaweza kutimia kama wataipigania au kuwashawishi viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuhakikisha kuwa timu ya JKT Mgambo itaufanya Azimio kuwa uwanja wake wa nyumbani.
0 comments

BREAKING NEWS !!!! MAITI YAKAMATWA NA KETE ZA MADAWA YA KULEVYA MOROGORO.


Maiti ikiwa ndani ya gari aina ya SPACIAL yenye namba ya usajili T 887 BSW eneo la nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospotali kuu ya mkoa wa Morogoro, baada ya gari hilo kukamatwa majira ya saa 7 usiku eneo la Mikumi,likiwa na watu watatu na maiti ya binadamu inayodaiwa kupoteza maisha baada ya kumeza kete hizo za zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya na kufariki dunia, ikisafirishwa kutoka Tunduma mkoani Mbeya kwenda Jijijini Dar es Salaam. PHOTO/MTANDA BLOG.

Polisi wakiendelea kupekua gari hilo.
HIZI ndizo kete zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya yaliyopatikana katika gari baada ya kupekuliwa kituo kikuu cha polisi.
0 comments

BREAKING NEWS: JAMES KISAKA AFARIKI DUNIA

 
KISAKA (KULIA) WAKATI AKIWA KAZINI SIMBA MSIMU ULIOPITA, WANAOMFUATIA NI NICO NYAGAWA, JULIO NA ABDALLAH KIBADENI
Kipa wa zamani na kocha wa zamani wa makipa wa Simba, James Kisaka amefariki dunia.

 
..WAKATI AKIWA MGONJWA NYUMBANI KWAKE MSASANI.
Kisaka amefariki dunia leo alfajiri na taarifa zinasema mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar.
Kisaka alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza upande mmoja kwa zaidi ya miezi miwili.
MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI
0 comments

RC GALLAWA AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA ZILIZOTOKA KWA JK KWA MAKAZI YA WAZEE WASIOJIWEZA MISUFINI MUHEZA.

RC GALLAWA AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA ZILIZOTOKA KWA JK KWA MAKAZI YA WAZEE WASIOJIWEZA MISUFINI MUHEZA.                    

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKISALIMIANA NA WAZEE WASIOJIWEZA WANAOISHI KATIKA KITUO CHA MSUFINI KATA YA NGOMENI WILAYANI MUHEZA LEO WAKATI ALIPOKWENDA KUKABIDHI ZAWADI ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA ZILIZO TOKA KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO

MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAKABIDHIANO HAYO LEO KABLA YA KUUMKARIBISHA MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA.

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA KITUO HICHO BAADA YA KUKABIDHI ZAWADI HIZO.

BAADHI YA VITU ALIVYOKABIDHI MKUU WA MKOA WA TANGA.

MKUU WA MKOA WA TANGA KULIA ALIYEINAMA AKIMKABIDHI MWENYEKITI WA KITUO HICHO JUMA BAKARI ZAWADI ZILIZOTOLEWA NA MH.RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA AJILI YA SIKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA KULIA AKISISITIZA JAMBO MARA BAADA YA KUKABIDHI ZAWADI HIZO KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA MUHEZA,SUBIRA MGALU.


ZAWADI ZA MBUZI ZILIZOKABIDHIWA KWENYE KITUO CHA KULELEA WAZEE WASIOJIWEZA CHA MSUFINI KATA YA NGOMENI WILAYANI MUHEZA AMBAZO ZILITOKA KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANI WA TANZANIA,DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE.PICHA ZOTE NA MBARUKU YUSUPH MUHEZA.

 MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa leo amekabidhi zawadi za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kutoka kwa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanga Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika eneo la makazi ya wazee wasiojiweza la Misufini kata ya Ngomeni wilayani Muheza

Zawadi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa Gallawa ni mchele kilo 150,mbuzi watatu(3) na Mafuta ya Chakula lita 40,michezo ya sabuni pamoja na katoni moja y chumivi vyote vikiwa na thamani ya sh.615,000.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, Gallawa ametoa wito kwa kila mwananchi kuweka utaratibu wa kusaidia wale wote ambao hawana uwezo na wenye shinda hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya krismas na mwaka mpya kama alivyofanya Mh.Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Aidha amewataka wananchi kushehereka sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa amani na utulivu kwa kuweka msisitizo kuwa wajiepueshe na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya husika pindi wanapoona katika maeneo yao kuna viashiria vya uvunjifu wa amani ikiwemo kuliweka jiji la Tanga katika hali ya usafi .

Wakati huo huo, Mkuu huyo wa mkoa ameaswa kuacha kuendesha magari mwendo kasi hasa katika kipindi cha sikukuu ya krismas na mwaka mpya kutokana na kuwa wananchi wengi hutumia vyombo vya usafiri kwenda mapumzikoni .
0 comments

WATU SABA WAKAMATWA KWA KUTUHUMIWA KUWEKA MABOMU YALIYOKUSUDIWA KULIPUA NYUMBA MBILI WILAYANI KOROGWE.

WATU SABA WAKAMATWA KWA KUTUHUMIWA KUWEKA MABOMU YALIYOKUSUDIWA KULIPUA NYUMBA MBILI WILAYANI KOROGWE.


 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Coastatine Massawe akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani silaa mbalimbali zilizokuwa zikutumiwa na watuhumuiwa waliokamatwa




 
 
Na Oscar Assenga,Korogwe.
JESHI la Polisi mkoani  hapa kwa kushirikiana na wakazi wa Kijiji cha Maili kumi wilayani Korogwe wamefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma za kuhusika na kuweka mabomu  yaliyokuwa yameandaliwa tayari kwa kulipuka kwenye nyumba mbili tofauti za ibada.
Pamoja na mabomu hao watuhumiwa hao ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi wanatuhumiwa kuhusika na kukutwa na vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko ya mabomu hayo pamoja na silaha za jadi ambazo pia zilikuwa zimefichwa katika nyumba hizo za ibada huku katika Kijiji cha Maili kumi wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Watu hao walikamatwa wakiwa na chupa 10 ambapo tano zilikuwa na  Petrol zikiwa na tambi zake ndani,gololi 103 ambazo hutumiwa kwa milipuko,galoni kubwa mbili zilizokuwa na lita nne za petrol,majambia,mishale yenye sumu,soksi za kuzuia uso(mask)upinde,Daftari lenye mafunzo ya kijeshi kuhusu namna kufungua na kufunga silaha.
Vifaa vingine ni mapanga,visu,Mifuko ya Sandarusi ,manati,vifuniko 12 vya maji,kofia nne na vitambaa vya kufunga kichwani pamoja na Tende walizokuwa wakitumia kama chakula.
Akizungumza  katika mahojiano na TANGA RAHA BLOG ofisini kwake leo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Constantine Massawe alisema kuwa watu hao walikamatwa Disemba 17 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku huko wilayani Korogwe.
Kamanda Massawe alisema kuwa Askari Polisi wakiwa kaika kizuizi cha Maili 10 wilaya ya Korogwe waliwatilia shaka vijana watatu wa kiume waliokuwa wamebeba vifurishi na walipotaka wasimame walikimbilia msituni na ndipo mmoja alipokamatwa na Askari hao.
“sasa baada ya kukamatwa huyu mmoja na ndipo alipopekuliwa na kukutwa na vifaa hivyo kwenye begi lake na ndipo msako wa kuwatafuta hawa wengine ulipoanza”,alisema Kamanda huyo.
Hata hivyo alisema kuwa  alisema kuwa katika msako huo ambao ulifanywa na Polisi kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la Maili kumi ndipo walipobaini kuwepo kwa vifaa vingine katika nyumba mbili tofauti za ibada zilizopo Kijijini hapo.
Alisema watuhumiwa hao baada ya mwenzao kukamatwa walikimbia kujificha kwenye nyumba hizo za ibada ndipo wakazi wa maeneo hayo walipowatilia mashaka na kutoa taarifa kwa Polisi.
“Baada ya kukimbizwa wakaona mahali salama kwao ni kwenye nyumba za ibada lakini wananchi wa eneo lile waliwatilia shaka na kuamua kutoa taarifa ndipo yalipokutwa hayo mabomu ambayo yalikuwa yameshaandaliwa kulipuka kwani kulikuwa na petrol na tambi ndani ya chupa hizo na zile gololi hutumika kama silaha zinapolipuka”,alifafanua Kamanda Massawe.
Hata hivyo kwa mujibu wa Kamanda huyo ni kwamba baada ya mahojiano ya Polisi na watuhumiwa hao walibaini kuwa ni miongoni mwa wale waliokimbi katika oparesheni ya kuwasaka wahalifu iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu huko wilayani Kilindi.
“Hawa ni miongoni mwa wale waliosababisha machafuko wilayani Kilindi ambapo Mgambo aliuawa sasa wengine walikimbia na inaonekana nao hawa wapo katika mtandao huo”,alisema.
Kamanda Massawe alitoa wito  kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kutoa taarifa mara moja kwa Polisi mara wanapobaini kuwepo kwa watu ambao wanawatilia mashaka kwenye maeneo yao.
0 comments

MAKAMBA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 2,JIMBONI KWAKE.

MAKAMBA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 2,JIMBONI KWAKE.                    

Na Rais Said,Lushoto.

 
NAIBU Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Technologia,Januari Makamba amemwaga vifaa vya michezo jimboni kwake vyenye thamani ya sh.milioni 2 lengo likiwa ni kuhamasisha vijana kupenda mchezo wa mpira wa miguu.
 
Vifaa vilivyotolewa na Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ni mipira 50 kwa vijana ikiwa ni harakati za kuhamasisha kuinua sekta ya michezo jimboni humo na kupata timu ambayo baadae itakuja kuwa tishio kwenye medani ya soka mkoani hapa.

 
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya mbunge,Katibu wa Mbunge huyo ,Hozza Mandia alisema vifaa vilivyotolewa ni katika kutekeleza ahadi zake alizozitoa kwa vijana jimboni humo kuwa atainua michezo kwa kutoa misaada kwa timu mbalimbali hasa za vijana.
 
 
Katibu huyo ambaye ni diwani wa kata ya Milingano alisema jitihada zinazofanywa na Makamba zinapaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa soka jimboni humo lengo likiwa kuwapa fuksa vijana kushiriki kwenye michezo.
 
   “Kama unavyojua michezo ni ajira ambayo inaweza kuwainua vijana na ni fursa ya kipekee kwao hivyo tunamshukuru Mh,Naibu Waziri kwa msaada huu kwani utaweza kuwaondoa vijana kukaa vijiweni ambapo muda mwingi hufikiria kufanya vitendo viovu badala yake watakuwa wakishiriki michezo kutokana na kuwa na vifaa vya kuchezea “Alisema Hozza.
 
Aidha katibu huyo alitoa wito kwa vilabu vya Mgambo Shooting na Coastal Union kuweka utaratibu wa kutembelea Jimboni humo ili kuweza kuangalia wachezaji wenye viwango vya hali ya juu ambao wanapatikana wilayani kuliko kuchukua wachezaji nje ya mkoa ambao wakati mwingine wanashindwa kuipa mafanikio timu hizo.
0 comments

PPF YAELEZA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TOKEA KUANZISHWA KWAKE.

PPF YAELEZA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TOKEA KUANZISHWA KWAKE.

Na Raisa Said,Handeni.
 Mfuko wa Pensheni wa PPF,umeeleza mafanikio yaliyopatikana kuanzishwa kwake kuwa ni pamoja na kuwalipia ada za masomo ya juu watoto yatima walioachwa na wazazi wao ambao ni wanachama wa mfuko huo kutokana na kufanya vizuri kwenye shule mbalimbali nchini. 
Meneja wa Kanda wa PPF, Zahra Kayugwa, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa tamasha la Handeni Kwetu lililofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.


"Tangu tulipoanzisha fao la elimu kwa wanachama waliokufa kwa watoto wao, limeonesha mafanikio makubwa kiasi cha kupelekea wengi wao kuendelea kusomeshwa na PPF hadi elimu ya juu"alisema Kayugwa.
Mfuko huo kwa mujibu wa takwimu alizozitoa jijini Tanga mwezi Septemba 2013, kwenye maonesho ya Kimataifa ya biashara, ambayo PPF ilishiriki kwa mara ya kwanza, zinaonyesha kwamba hadi kufikia Desemba mwaka jana, ulikuwa umetumia kiasi cha shilingi milioni 682.9 kusomesha wanafunzi wapatao 1,333 kote nchini.

Zahra akielezea changamoto zinazoukabili mfuko huo, ni suala la uwekezaji wa nyumba ambapo wanapotaka kujenga nyumba za gharama nafuu, mamlaka zinazohusika katika miji huwa zinawauzia bei kubwa kuliko uwezo wa mfuko hatua ambayo, wanashindwa kuendelea na kasi ya ujenzi wa nyumb

a hizo.
"Kwa kweli mfuko umekuwa na nia njema kabisa ya kuendelea kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wanachama wake, lakini tatizo kubwa tunakatishwa tamaa na mamlaka za miji hapa nchini, tunapotaka ardhi kwa ajili ya kujenga nyumba hizo bei yake inakuwa kubwa kuliko maelezo," alisema Zahra ambaye anashuhghulika na mikoa ya Kinondoni, Pwani na Tanga.

Hata hivyo, alisema pamoja na hali hiyo bado mfuko huo, unajipanga kuhakikisha unajenga nyumba hizo na kwamba kwa sasa wanajenga katika mikoa ya Mwanza, Pwani, Mtwara, Iringa, na Dar es salaam ambapo pia wamekuwa wakifungua ofisi za mikoa kwa lengo la kuwahudumia wateja wao.
0 comments

TASWIRA YA MAPOKEZI YA MHE ZITTO ZUBERI KABWE NAMNA ALIVYOPOKELEWA HIVI PUNDE KIGOMA

TASWIRA YA MAPOKEZI YA MHE ZITTO ZUBERI KABWE NAMNA ALIVYOPOKELEWA HIVI PUNDE KIGOMA

Mbunge wa Kigoma kaskani Mh Zitto Kabwe akisalimiana na wakazi wa Kigoma mara baada ya Kuwasili kigoma asubuhi ambapoa wakazi wa kigoma wamejitokeza kwa wingi kumpokea Mbunge wao.

Zitto Kabwe akiwa katika gari la wazi mara baada ya kutua kigoma asubuhii ambapo amepata mapokezi ya kishindo


wafuasi wa Zitto kabwe wakiwa katika maandamano..
 

































0 comments

BASI LA ALLYS YAUA ABIRIA SABA JANA USIKU BUHONGWA-MWANZA.


Basi la kampuni ya Allys Sport Bus linalosafirisha abiria kutoka Dar es Salaam na Mwanza likiwa limeacha njia na kupinduka baada ya kutokea ajali inayodaiwa kusababishwa na basi la Shabiby lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani Morogoro. PICHA MAKTBA/MTANDA BLOG.  WATU saba wamekufa papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa baada ya basi la Allys linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam hadi Mwanza kugongana uso kwa uso na daladala katika eneo la Buhongwa mkoani Mwanza.
0 comments

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHAFANYIKA MKOANI TANGA LEO.

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHAFANYIKA MKOANI TANGA LEO.

 katikati waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Mh Ddkt Terezya Huvisa kulia ni katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula na kushoto ni katibu mpya wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Isaya Kisiri,katika kikao cha Baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo mjini Tanga leo.
Waliokaa, katikaTi ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza jipya la wafanyakazi la Ofisi hiyo jijini Tanga leo..
 Wajumbe wa baraza jipya la wafanyakazi kutoka ofisi ya makamu wa rais katika kikao cha baraza hilo mjini tanga leo.
.Picha na Evelyn Mkokoi.
0 comments

WAGANDA WAHOJI FIFA OKWI KWENDA YANGA




Uongozi wa Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) umendika barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutaka kujua uhakika kuhusiana na mshambuliaji Emmanuel Okwi kuuzwa Yanga.

Taarifa zinasema katika mtandao wa MTNfootball kwamba OKwi alijiunga na Yanga kwa kitita cha sola 100,000 lakini Fufa kupitia bosi wake, Edgar Watson imetaka kujua uhalali kuhusiana na uhamisho wake.

Fufa kupitia Watson imetaka kujua kama ni sahihi kwa kuwa kwamba ni sahihi Okwi aliyepelekwa SC Villa kwa mkopo akitokea Etoile du Sahel ya Tunisia kama anaweza kucheza Yanga.

Okwi alidumu SC Villa kwa miezi miwili akiichezea timu hiyo katika Ligi Kuu ya Uganda na kufanikiwa kufunga mabao matatu.

Lakini Mkurugenzi we SC Villa, Edgar Agaba ameiambia MTNFootball.com, Okwi alikuwa mchezaji huru kabla ya kwenda kujiunga na Yanga.

Okwi amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu na kusababisha vurugu kubwa hasa Simba wanapinga kwa kuwa wanahitaji kulipwa fedha zao dola 300,000 kutoka Etoile du Sahel.
0 comments

AZAM FC WAFUNGA 'SOFA ZA HATARI' CHAMAZI, KOMBE LA SHIRIKISHO PALE PALE MWAKANI

AZAM FC WAFUNGA 'SOFA ZA HATARI' CHAMAZI, KOMBE LA SHIRIKISHO PALE PALE MWAKANI

Mafundi wakiendelea na zoezi la uwekaji wa viti vya kisasa katika majukwaa ya Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Klabu ya Azam inataka kuutumia Uwanja huo kwa michuano ya Afrika pia mwakani na inapambana na muda kuhakikisha uboreshaji unakamilika mapema ili mechi zake za Kombe la Shirikisho icheze hapo mwakani.
Siti za kulala
Hiki ni moja ya vyumba vya kubadilishia nguo kwa ajili ya timu, unaweza kujionea ni cha kisasa kabisa
Mafundi wamemaliza kazi ya kupaka rangi na sasa mabinti wanafanya usafi
Chumba cha mikutano, ni cha hadhi ya juu
Eneo hili ndilo timu zitakuwa zinatokea kuingia uwanjani
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger