Handeni wazitamani Simba na Yanga kukipiga kwenye Uwanja wa Azimio wilayani kwao
Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa
Handeni
MKURUGENZI wa Halmashauri ya
Mji wa Handeni, mkoani Tanga, Thomas Mzinga, amesema kwamba Uwanja wao wa
Azimio unastahili kukutanisha vigogo vya Simba na Yanga, katika michuano yoyote
nchini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, pichani.
Akizungumza na Handen Kwetu Blog mapema wiki hii wilayani Handeni, Mzinga alisema kuwa hiyo ni kutokana
na maandalizi na mwonekano wa uwanja wao wa michezo.
Alisema kuwa Uwanja wao ni
mkubwa na unastahili kukutanisha timu kubwa na vigogo wa Tanzania Bara,
vikiwapo Simba na Yanga.
“Tunajivunia kuwa na uwanja
mzuri na muwajulishe huko kuwa wanapaswa waje wacheze huku katika mashindano yao mbalimbali.
“Tunaamini Uwanja huu pia
ukikamilika kwa baadhi ya ukarabati wake, basi utachangia kwa kiasi kikubwa
kuleta watu mbalimbali, hasa timu kubwa zitakapokuja,” alisema Mzinga.
Hata hivyo, kiu ya Mzinga na
viongozi wa serikali wilayani humo inaweza kutimia kama
wataipigania au kuwashawishi viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),
kuhakikisha kuwa timu ya JKT Mgambo itaufanya Azimio kuwa uwanja wake wa
nyumbani.
Post a Comment