PPF YAELEZA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TOKEA KUANZISHWA KWAKE.
Na Raisa Said,Handeni.
Mfuko
wa Pensheni wa PPF,umeeleza mafanikio yaliyopatikana kuanzishwa kwake
kuwa ni pamoja na kuwalipia ada za masomo ya juu watoto yatima
walioachwa
na wazazi wao ambao ni wanachama wa mfuko huo kutokana na kufanya vizuri
kwenye shule mbalimbali nchini.
Meneja wa Kanda
wa PPF, Zahra Kayugwa, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa tamasha
la Handeni Kwetu lililofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali.
"Tangu tulipoanzisha fao la elimu kwa wanachama
waliokufa kwa watoto wao, limeonesha mafanikio makubwa kiasi cha kupelekea wengi wao
kuendelea kusomeshwa na PPF hadi elimu ya juu"alisema Kayugwa.
Mfuko huo kwa mujibu wa takwimu alizozitoa jijini Tanga mwezi Septemba 2013, kwenye maonesho ya Kimataifa ya biashara, ambayo PPF ilishiriki kwa mara ya kwanza, zinaonyesha kwamba hadi kufikia Desemba mwaka jana, ulikuwa umetumia kiasi cha shilingi milioni 682.9 kusomesha wanafunzi wapatao 1,333 kote nchini.
Zahra akielezea changamoto zinazoukabili mfuko huo, ni suala la uwekezaji wa nyumba ambapo wanapotaka kujenga nyumba za gharama nafuu, mamlaka zinazohusika katika miji huwa zinawauzia bei kubwa kuliko uwezo wa mfuko hatua ambayo, wanashindwa kuendelea na kasi ya ujenzi wa nyumb
a hizo.
"Kwa kweli mfuko umekuwa na nia njema kabisa ya kuendelea kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wanachama wake, lakini tatizo kubwa tunakatishwa tamaa na mamlaka za miji hapa nchini, tunapotaka ardhi kwa ajili ya kujenga nyumba hizo bei yake inakuwa kubwa kuliko maelezo," alisema Zahra ambaye anashuhghulika na mikoa ya Kinondoni, Pwani na Tanga.
Hata hivyo, alisema pamoja na hali hiyo bado mfuko huo, unajipanga kuhakikisha unajenga nyumba hizo na kwamba kwa sasa wanajenga katika mikoa ya Mwanza, Pwani, Mtwara, Iringa, na Dar es salaam ambapo pia wamekuwa wakifungua ofisi za mikoa kwa lengo la kuwahudumia wateja wao.

Post a Comment