skip to main |
skip to sidebar
Mwakilishi wa UK Sports atembelea Wizara ya Habari
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo akifafanua jambo
wakati wa mkutano wake na Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la
Uingereza Bwana Elias Musangeya (kushoto) alipotembelea Wizarani hapo
kwa ajili ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration
leo jijini Dar es Salaam.
pix2: Katibu Mtendaji wa Baraza la
Michezo la Taifa Henry Lihaya (kushoto) akielezea jambo huku Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard
Thadeo (kulia) na Mshauri Mwandamizi wa UK Sports Elias Musangeya
(katikati) wakimsikiliza kwa makini. Mkutano huo umefanyika ikiwa ni
sehemu ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration.(P.T)
pix3: Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo (kulia) na Mshauri
Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza Bwana Elias Musangeya
(kushoto) wakifurahia jambo walipokutana ofisini kwa Kaimu Katibu Mkuu
huyo kwa ajili ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International
Inspiration leo jijini Dar es Salaam.
pix4: Kutoka kulia Kaimu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo,
Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza Bwana Elias
Musangeya, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya na
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo sehemu ya Usajili Bi. Mercy
Rwezahura wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha
tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration
kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija - WHVUM
Copyright © 2011.
TANGA LEO - All Rights Reserved
Post a Comment