SIMBA SC YAMSIMAMISHA RAGE, SASA NI VURUGU TUPU MSIMBAZI

SIMBA SC YAMSIMAMISHA RAGE, SASA NI VURUGU TUPU MSIMBAZI

Na Mahmoud Zubeiry, Kariakoo
KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC kilichokutana jana, kimefikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage kwa kukiuka taratibu na maadili ya uongozi.
Rage amesimamishwa siku mbili tu baada ya kusajili wachezaji wawili wapya, akiwemo Awadh Juma pichani

Simba SC imeitisha Mkutano na Waandishi wa Habari ambao utafanyika saa 5:30 makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam kuelezea kwa undani suala hilo.
Wazi hatua hii inazidi kuivuruga klabu, kwani tayari aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ naye amejiuzulu na nafasi yake inashikiliwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Itang’are ‘Kinesi’.
Maana yake Simba SC inaendeshwa bila kiongozi Mkuu wa kuchaguliwa na hiyo inaweza kushinikiza uchaguzi haraka. 
HABARI ZAIDI ZITAFUATIA BAADA YA MKUTANO WA KLABU NA WAANDISHI WA HABARI.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger