Coastal Union U20 yaanza vema michuano ya Uhai.
Nzara Ndaro akiangalia wa kumpa mpira katika kipindi cha kwanza wakati huo timu imelala 1-0.
Ayoub, beki mbili wa Coastal Unio akitoa pasi kwa Raizin Hafidh (namba nne) huku Nzara Ndaro (nahodha wa Coastal) akiangalia kwa makini.
Kiungo mshambuliaji wa Coastal Union Ally Ufudu akikokota mpira kuelekea lango la Azam.
Yusuf Chippo akiwajibika uwanjani, hapa anawakemea vijana wake wasicheze mipira ya juu.
Tunakwenda moja moja, ndiyo staili ya kocha Yusuf Chippo.
Balaaaa... mchezaji mmoja anakabwa na kijiji.
Penalt hii iliyoingizwa kimiani na Raizin Hafidh 'Boban' dakika ya 50 baada ya mchezaji wa Azam kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Wachezaji wa Coastal Union wakishangilia bao la kwanza lililofungwa kwa mkwaju wa penalt dakika ya 50.
Nao ni na...
Raizin Hafidh 'Boban' akiwa ameshampiga chenga golikipa wa Azam, anaelekea kupiga shuti kwa guu lake la kushoto kuhitimisha kilio kwa Azam dakika ya 55.
Wachezaji wa Coastal Union wakishangilia bao la pili lililofungwa na Raizin Hafidh 'Boban'.
Raizin Hafidh 'Boban' akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Azam huku mchezaji wa Coastal akiwa tayari kutoa msaada.
Kocha wa Coastal Union, Yusuf Chippo akizungumza na kiungo wa timu hiyo
Ally Ufudu wakati mechi ikiendelea, leo asubuhi uwanja wa Karume Ilala
jijini.
TIMU ya Coastal Union chini ya miaka 20 imeanza vema
michuano ya UHAI U20 baada ya kuwachapa mahasimu wao wa muda mrefu Azam FC kwa
mabao 2-1 yaliyoingizwa kimiani na kijana
Ilikuwa ni dakika ya 50 kipindi cha pili baada ya mchezaji
wa Azam kuunawa mpira katika eneo la hatari Raizin Hafidh ‘Boban’ akakabidhiwa
mikoba ya kupiga mkwaju wa penalt ambao ulitikisa nyavu za Azam huku golkikipa
wa timu hiyo akibaki chini ameshangaa.
Bao hilo liliamsha shangwe katika uwanja wa Karume uliopo
Ilala jijini Dar es Salaam, hali iliyoonyesha watazamaji wengi walikuwa upande
wa Coastal Union.
Baada ya bao hilo kuingia wachezaji wa Azam walipoteza
mwelekeo na kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwao hali iliyompa
mwanya ‘Boban’ ambaye alitokea upande wa kulia akamramba chenga beki wa Azam
akaingia kwenye box dogo akakutana na golikipa wa Azam amezubaa, naye akamramba
chenga na kumalizia kazi nzuri iliyotokana na juhudi zake binafsi kwa mguu wa
kushoto.
Kuingia kwa bao la pili kulimaanisha kitu kimoja tu kwa
Azam, kuhakikisha mvua hiyo ya mabao haiendelei. Hivyo wakaanza kucheza mchezo
wa kujihami hali iliyowafanya kuendelea kushambuliwa mara kwa mara.
Hata hivyo wachezaji wa Coastal Union nao wakaanza kujisahau
na kucheza kwa kujiamini huku wakionekana kuridhika na mabao hayo. Kutokana na
mchezo huo ulioonyesha dharau na kujiamini vijana hao ambao mwaka jana
walitawazwa kuwa kikosi bora cha michuano hiyo, walikosa mabao mengi ya wazi yaliyosababishwa
na uzembe wa mabeki wao.
Katika kipindi cha kwanza Azam ambao ni mabingwa watetezi wa
michuano hiyo baada ya kuwatoa Coastal Union mwaka jana walipata bao la mapema
katika dakika ya 3 mfungaji akiwa Erick Haule, aliyetumia vema makosa ya mabeki
wa Coastal Union na kumalizia krosi iliyopigwa kutoka upande wa kulia ikamkuta
miguuni na kumbabatiza golikipa wa Coastal Union kasha ukaingia wavuni.
Bao hilo lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza huku
vijana wa Coastal Union wakiomba kipindi hicho kiishe mapema kutokana na
mashambulizi waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa wapinzani wao.
Katika hatua nyingine, ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC
ndiwo ushindi wa kwanza kwa Coastal Union chini ya miaka 20 kwa vijana wenzao
hao tangu walipoanza kukutana miaka minne iliyopita.
Aidha kwa mara tatu mfululizo Azam wamekuwa wakiwashinda
Coastal Union kwa mikwaju ya penalt kwenye hatua ya mtoano, baada ya kutoka
suluhu kwenye dakika za kawaida.
Kundi A lina timu nne za Coastal Union, Azam FC, Yanga na
Mbeya City. Matokeo ya mechi inayochezwa sasa kati ya Yanga na Mbeya City ndiyo
yataihakikishia Coastal Union kuongoza kundi kabla ya kutupa karata yake ya
pili siku ya Jumanne dhidi ya Yanga katika uwanja wa Karume Ilala saa mbili
asubuhi.
COASTAL UNION
NOV 17, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Post a Comment