Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Antony Komu- Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare- Kagera.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila- Dodoma.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John John Mnyika- Mwanza
Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema- Kilimanjar.o
Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala- Morogoro.
Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao
Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa
kwa kufuata taratibu za chama.
Hii ni kwa sababu maboresho
yanayofanyika ndani ya chama, hadi sasa yanaendelea katika ngazi ya
Makao Makuu na kanda, kisha itaendelea kwa ngazi za mikoa, wilaya,
majimbo, kata, kijiji na hatimaye kitongoji.
Katika maboresho hayo, kwa nafasi za
uteuzi, yanayoendelea sasa ambayo yanakwenda hatua kwa hatua, hadi kuwa
na makatibu wa kuajiriwa ngazi ya chini ya chama, chama kinazingatia
uwezo, uadilifu na utayari wa mtu katika kutoa utumishi bora kwa
wanaCHADEMA na Watanzania wote katika nafasi husika.
Suala la maslahi ya watumishi wa
CHADEMA ni utaratibu wa chama ambao unajadiliwa, kufikiwa uamuzi na
kisha kuridhiwa kwenye vikao vya chama, kama ilivyofanyika kwenye kikao
cha Kamati Kuu kilichoketi karibuni.
Katika suala hili la maslahi ya
watumishi wanaojitolea Makao Makuu ya CHADEMA ambayo si siri, Ndugu
Chitanda amesema uongo mkubwa. Kusema kwamba Ofisa Mwandamizi anaweza
kulipwa posho kubwa kuliko Mkurugenzi wa kurugenzi husika, ni uongo
unaovuka mipaka.
Ndugu huyo anadhihirisha uongo huo
yeye mwenyewe kwa kuandika hivi; "800,000/= za awali na sasa itakuwa ni
kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka
Tshs.6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni
Tshs.1,000,000-1,500,000/=".
Pia si kweli kuwa kila mtumishi
anayejitolea Makao Makuu analipwa. Mathalani, wakurugenzi wenye nafasi
za ubunge, hawalipwi hata shilingi moja kwa kazi zote wanazokitumikia
chama na Watanzania kwa ujumla.
Kwa maelezo hayo ya kutengeneza, ni
kwamba hadi sasa Ofisa Mwandamizi anapokea posho kubwa kuliko Mkurugenzi
na hata baada ya maboresho atapata posho kulingana na Mkurugenzi.
Anapaswa kuwa mkweli. Mtu anayetaka kuonekana muungwana, anapaswa
kujiweka mbali na uongo pamoja, maneno ya kutunga pamoja na upotoshaji
wa makusudi.
Kama ilivyoelezwa hapo juu,
restructuring inaendelea. Ni hatua kwa hatua. Itafika ngazi za chini
kama Baraza Kuu lilivyoagiza. Kwa sababu hiyo hadi sasa uteuzi wa
Makatibu wa Mikoa na Wilaya haujafanyika.
Hata hivyo ruzuku imekuwa ikipelekwa
kila kanda, mkoa, wilaya na jimbo kama ilivyoridhiwa na Kamati Kuu. Na
hii ni zaidi ya pikipiki, kompyuta na magari yaliyopelekwa kila kanda.
Angelikuwa mkweli, nagelisema na hili pia.
Ndugu Chitanda anajichanganya sana
katika taarifa yake yote. Hii ni moja ya sifa ya kukosa hoja hivyo mtu
anaamua kuibua viroja au kutunga maneno kwa sababu ya kujaribu kuukana
ukweli anaoujua moyoni. Tutatoa mfano mmoja;
Kupitia taarifa yake, anasema alikuwa
mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo
anasema kuna ubaguzi! Tunapaswa kumhurumia kwa kushindwa kuunganisha
hata mawazo yake na kupata mtiririko wa hoja zenye mantiki! Angelikuwa
mkweli angesema katika vikao vya sekretarieti na CC, aliingiaje kama
kuna ubaguzi wa dini!
Kwa sababu anazozijua yeye, Ndugu
Chitanda ameamua kujipachika cheo ambacho hajawahi kuwa nacho. Amejiita
kuwa ni Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu.
Ndani ya CHADEMA pamoja na kwamba
nafasi hiyo imetajwa ndani ya Katiba ya Chama, hakuna mtu ambaye
ameteuliwa kutumikia nafasi hiyo. Kama anaweza athibitishe kwa kutoa
barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu.
Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni
Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja
ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa CHADEMA.
Operesheni ya Chama inayoendelea nchi nzima kwenye majimbo 103, si suala la siri wala lengo bovu kama anavyotaka umma uamini.
Ni mwendelezo wa mpango mkakati wa
chama kupitia progamu za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), unaotekelezwa kwa
hatua mbalimbali na kwa mbinu tofauti tofauti pamoja na dhana ya
CHADEMA ni msingi.
Operesheni hiyo ambayo ni mwendelezo
wa nyingi za namna hiyo zinazokwenda ngazi za chini kabisa za chama,
zikilenga kuimarisha taasisi na mifumo, imeanza wiki hii na ilitangazwa
mbele ya waandishi wa habari.
Tungependa kumalizia ufafanuzi huu
mfupi kwa kutoa tahadhari kwa umma kuwa makini na matamko ya watu wa
namna hii. Maana tunajua kwa uhakika yako mengi ya namna hii
yataandaliwa na kutolewa kadri ambavyo Watanzania wanakaribia kuona na
kuishi matumaini ya mabadiliko ya kiutawala na mfumo ndani ya nchi yao.
Mathalani katika taarifa yake, Ndugu
Ali Chitanda amedhihirisha na kuonesha kuwa ni aina ya watu ambao
wanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuwaangalia kwa macho ya
kuhoji na tahadhari ya hali ya juu, anasema hivi;
"Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa
nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa
ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi,
ubaguzi wa kikabila na kikanda."
Aya hiyo pekee inayotumia lugha
wanayotumia mahasimu wa CHADEMA, wakiongozwa na viongozi waaandamizi wa
CCM, wanaohangaika kutokana na Watanzania kuwakataa, wakijiandaa
kuwaondoa madarakani kwa sababu sera zao zimeshindwa, inatosha kuonesha
uhalisia wa yeye mwenyewe (mtoa taarifa) alivyo.
Ni kauli za namna hii (kuwatisha na
kutaka kuwatenganisha Watanzania) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watawala
kama njia pekee ya kutaka kuzuia upepo wa mabadiliko unaovuma nchi
nzima, zimekuwa zikiwaunganisha zaidi Watanzania kuiunga mkono CHADEMA
bega kwa bega, ili kupata haki na matumaini ya wanyonge, katika
mapambano ya awamu ya pili, kuelekea uhuru wa kweli.
Imetolewa leo Novemba 30, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
Latest Post
CHADEMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA
CHADEMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA
Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu Ali Omari. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;
Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, chama kimeshafunga mjadala kwenye vyombo vya habari kwa kuheshimu na kuzingatia taratibu za kikatiba za ndani ya chama kuendelea.
Pili kuhusu suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya;
1.Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika
3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.
Kama ni suala la kuangalia mtu anatokea wapi (ambalo halijawahi wala haliwezi kuwa moja ya vigezo), ili kuonesha ukweli na kubainisha uongo wa watu wanaojaribu kufanya kazi ya CCM wakisema wao ni wanaCHADEMA, kwa kutumia propaganda zile zile na kuzifanya kuwa ni kete zao za kisiasa ndani ya chama, tunaweza kutaja maeneo ya wanakotoka au asili yao kama ifuatavyo;(P.T)
ARSENAL HAIKAMATIKI, YAWAFUMUA CARDIFF 3-0 BARAZANI KWAO...LUKAKU NI HATARI
ARSENAL HAIKAMATIKI, YAWAFUMUA CARDIFF 3-0 BARAZANI KWAO...LUKAKU NI HATARI
Ramsey hakutaka kushangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani
Mabao ya Arsenal yamefungwa na Aaron Ramsey dakika ya 29 akimalizia pasi ya Mesut Ozil na 90 pasi ya Theo Walcott na Mathieu Flamini dakika ya 86 pasi ya Ozil tena.
Ushindi huo, unaifanya Arsenal itemize pointi 31 baada ya kucheza mechi 13, ikiizidi Liverpool iliyo katika nafasi ya pili kwa pointi saba.
Lukaku akishangilia bao lake leo
Everton imeichapa 4-0 Stoke City Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, mabao ya Gerard Deulofeu dakika ya 45, pasi ya Gareth Barry, Seamus Coleman dakika ya 49 pasi ya Barry tena, Bryan Oviedo dakika ya 58, pasi ya Gerard Deulofeu na Romelu Lukaku dakika ya 79 pasi ya Oviedo.
Bao pekee la Gary Hooper dakika ya 30 limeipa Norwich ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Carrow Road, Norwich, Norfolk.
West HamUnited imeifunga 3-0 Fulham Uwanja wa Boleyn Ground, London mabao ya Mohamed Diame dakika ya 47, Carlton Michael Cole Okirie dakika ya 82 na Joe Cole dakika ya 88.
Aston Villa imetoka sare ya bila kufungana na Sunderland Uwanja wa Villa Park na mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England, Newcastle United imeifunga West Bromwich 2-1.
KOCHA WA CAMEROON ASAINI MIAKA MWILI AZAM
KOCHA MCAMEROON ASAINI MIAKA MWILI AZAM
Kocha mpya wa Azam FC. Joseph Marius Omog (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
KLABU ya Azam inapenda kuufahamisha umma hususan
wapenzi wa mpira wa miguu kuwa imeingia mkataba na kocha Joseph Marius Omog
raia wa Cameroon kwa kipindi cha miaka miwili (2) kuanzia leo.
Kocha Omog ni bingwa kwani anakuja kuifundisha Azam
akiwa ametoka kuiongoza klabu ya A.C Leopards ya Jamhuri ya Kongo (Brazaville)
kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013).
Timu hii ilikuwa haijatwaa ubingwa wa ligi kwa zaidi
ya miaka 30. Kwa mwaka huu wametwaa ubingwa wakiwaacha wapinzani wao, Diables
Noirs kwa pengo la pointi kumi (10) wakikusanya pointi 87 katika ligi yenye
timu 18.
Pia ni mwaka jana tu (2012) aliiwezesha A.C Leopards
kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika kwa kuzipiga kumbo timu ngumu
na zenye uzoefu mkubwa kama vile Mas de Fes ya Morocco, Heartlands ya Nigeria
na Sfaxien ya Tunisia.
Mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa wa Afrika
yalifikiwa baada ya miaka 38 tangu klabu ya Jamhuri yas Kongo ifanye hivyo, na
kumfanya kocha Omog kuwa moja ya makocha wa kupigiwa mfano barani Afrika.
LAAC WAIAGIZA HALMASHAURI HANDENI KUPELEKA ZAIDI YA MILI 105 KWA VIJIJI RUZUKU YA SERIKALI.
LAAC WAIAGIZA HALMASHAURI HANDENI KUPELEKA ZAIDI YA MILI 105 KWA VIJIJI RUZUKU YA SERIKALI.
Kauli ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo ilitokana na halmashauri hiyo kushindwa kuzipeleka vijijini fedha za ruzuku ya serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo hali ambayo inapelekea kuchangia kudhorotesha kasi yao katika shughuli mbalimbali.
Licha ya kutoa agizo hilo
pia aliiagiza halmashauri hiyo kuandaa mchanganuo wa madeni inayodai na kudaiwa
kwa kuonyesha majina ya wadai na wadaiwa ikiwemo kuchukua hatua za makusudi za
kupatikana kwa fedha zinazodaiwa.
Mwenyekiti huyo alisema katika mchanganuo huo wadai wa halmashauri unaonyesha ni kiasi cha sh.milioni 736,302,302 ambapo katika hilo mchanganuo wa wadaiwa hao haukuonyesha kitendo ambacho kinaleta mashaka hasa katika utendaji wake.
Aidha pia kamati hiyo iliagiza mchanganuo wa matumizi ya
mabati 466 yaliyotumika kujengea vyumba 8 vya madarasa katika shule ya
sekondari Segera uandaliwe na kupelekwa kwa mkaguzi mkazi kwa ajili ya uhakiki
zaidi.
Aliitaka halmashauri hiyo kuzingatia vipimo na vigezo vya
ubora katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi ambapo agizo hilo lilitokana na kubainika kwa kiwango duni
kwa madarasa manne yaliyojengwa kwa sh.milioni 14 katika shule ya sekondari
Komnyang’anyo.
Hata hiyo waliitaka halmashauri hiyo kuongeza bidii katika
kudai kiasi cha sh.,milioni 133,391,724 ambazo inadai kutoka kwa wadaiwa ambao
ni pamoja na MSD sh.milioni 39,310,646,State Business sh.milioni
14,690,000,HADECO sh.milioni 10,200,000, Hazina (15% LAPF) sh.milioni
44,059,300, Hazina(Salaries)sh.milioni 19.806,278 na mfuko wa wanawake ni
sh.milioni 5,025,500.
Kigoda: Kamanda wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM)
Kigoda: Kamanda wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM)
WAZIRI wa Biashara na Viwanda
nchini, Dr.Abdalla Kigoda ameteuliwa kuwa kamanda wa Umoja wa Vijana Mkoa wa
Tanga (UVCCM) katika uteuzi ambao ulifanywa na kamati ya utekelezaji Taifa
chini ya Mwenyekiti wao Sadifa Juma.
Akizungumza na Tanga Raha, katika ofisi
za Umoja huo mkoani hapa, Mwenyekiti wa Umoja huo, Abdi Makange alisema
mchakato huo ulianzia ngazi ya mkoa ambapo wao waliamua kumpendekeza Kigoda na
hatimaye kupata baraka kutoka kamati ya utekelezaji na kumuidhinisha kwa
kumpitisha.
Makange alisema hatua yao ya kumpendekeza ilitokana na mchango wake mkubwa aliokuwa ukitolewa na kiongozi huo kwa vijana wa mkoa wa Tanga kitendo ambacho kimewapa wigo katika ufanisi wao.
“Naishukuru sana kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa
kuridhia mapendekezo hayo na sasa tunakwenda kufungua ukurasa mpya wa mafaniko
ndani yetu “Alisema Makange.
Alisema umoja huo unatarajiwa
kuandaa taratibu za kumsimika rasmi kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Handeni mkoani Tanga lengo likiwa ni kuhakikisha wanatimiza malengo yao waliojiwekea.
Harufu ya ufisadi yabainika halmashauri za Tanga
Harufu ya ufisadi yabainika halmashauri za Tanga
Jiji la Tanga
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa LAAC, Rajabu Mbarok, katika majumuisho ya ziara yao katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Tanga na kushirikisha wakuu wa idara, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri, mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya.
Mbarok alimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bendkito Ole Kuyani, kuunda kamati ya kuchunguza suala hilo huku akitaka mwenyekiti huyo asimamishwe kazi ili kuepuka kuharibu uchunguzi.
Mbarok alisema wametembelea miradi sita katika halmashauri hiyo ikiwamo soko la kimataifa linalojengwa maeneo ya Makuyuni na kwamba miradi hiyo hairidhishi na kutolea mfano choo kilichojengwa kwa thamani ya Sh. milioni saba ambacho hakilingani na thamani halisi ya fedha.
Alisema halmashauri ya Korogwe imekuwa ikipata hati chafu kwa muda wa miaka mitano sasa na zaidi ya Sh. bilioni moja hazikutumika.
Kuhusu halmashauri ya Mji Mdogo wa Korogwe, alisema walikagua miradi mitano, lakini miradi yenye nafuu ni miwili tu hiyo mingine ipo chini ya viwango huku akimpa onyo mkurugenzi wa mji wa Korogwe kwa kuikimbia kamati hiyo na kwenda kujificha na kuwa wamekaidi agizo la mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa hawawapandishi vyeo walimu na kuwaongezea mishahara mpaka sasa.
Katika Jiji la Tanga alisema walikagua mradi wa bwawa la umwagiliaji liliyopo Mabaayani lakini aligundua ufisadi mkubwa na kusema kuwa mradi huo ni wa watendaji na sio wananchi kwani mpaka sasa zaidi ya MSh. mlioni 300katika mradi huo zimeliwa na wajanja.
Tanga sasa hatarini kupoteza hadhi ya Jiji
Tanga sasa hatarini kupoteza hadhi ya Jiji
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Chiku Gallawa
Hayo yalibainishwa jana na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati wa majumuisho ya ziara yao.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajabu Mbaruk, alisema kamati inakwenda kuishauri serikali kushusha hadhi ya kuwa jiji na kurudi katika hadhi ya manispaa kwa kuwa imeshindwa kukusanya mapato.
Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Tanga inatia aibu kwani inakusanya mapato ya Sh. bilioni 3.5 kwa mwaka ambayo ni madogo kulinganisha na ya Jiji la Mwanza ambalo linakusanya Sh. bilioni 10 kwa mwaka.
Alisema cha kusangaza, Halmashauri ya Jiji la Tanga ina vyanzo vingi vya mapato, lakini mapato hayakusanywi na kusema kuwa hiyo ni aibu na haifai kuwa na hadhi ya jiji.
Mbarok alisema kuwa madiwani na watendaji hawana uchungu na halmashauri ya jiji la Tanga. “Sasa kamati inakwenda kuishauri serikali kushusha hadhi jiji la Tanga kuwa manispaa kama zamani,” alisema.
Alisema kuwa Mkoa wa Tanga una wilaya tisa, lakini cha kushangaza ni kuwa mkoa mzima wanakusanya Sh. bilioni nane tu na kuzidiwa na Jiji la Mwanza.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kiasi cha Sh. bilioni mbili za mapato zimepotea kutokana na jiji hilo kutokuwa na uwezo wa kutunza vizuri kumbukumbu za mahesabu.
Alipoulizwa na NIPASHE kuhusiana na lini LAAC itakutana na serikali ili kuwasilisha pendekezo la kulishusha hadhi Jiji la Tanga, alisema kamati yake inaandaa taarifa ya mapendekezo na ili kuipeleka Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi).
CHANZO:
NIPASHE
Waziri Kigoda mgeni rasmi tamasha la Handeni Kwetu 2013
Waziri Kigoda mgeni rasmi tamasha la Handeni Kwetu 2013
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Viwanda na Biashara ambaye pia ndio mbunge
wa Handeni, Dkt Abdallah Kigoda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la
Utamaduni, lililopangwa kufanyika Katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni
mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda, pichani.
Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani hapa,
huku likitarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayoendelea
kushika kasi.
Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo,
Kambi Mbwana, alisema maandalizi yamezidi kushika kasi kwa kuangalia mazoezi ya
vikundi kadhaa vitakavyotoa burudani katika tukio hilo.
“Tunashukuru Mungu kuona mambo yanazidi kuwa mazuri kwa
kuhakikisha kuwa Desemba 14 mwaka huu tunafanya tamasha lenye mguso na kila
mmoja wetu kufaidishwa.
“Huu ni wakati wa kila mtu kujipanga ili aje kushiriki kwa
namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa juhudi hizi zote zipo kwa ajili ya
kujenga ushirikiano kwa watu wote,” alisema Mbwana.
Wadhamini katika tamasha hilo ni pamoja na gazeti la Mwananchi,
Clouds Media Group, ni Phed Trans, Clouds Media
Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah
Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS
(T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi
Media Group duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters
chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati
Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com,
huku likipangwa kuanza saa 2 za asubuhi hadi saa 12 za jioni.
CHADEMA TANGA YAPONGEZA UAMUZI WA KUVULIWA UONGOZI KATIBU MSAIDIZI
CHADEMA TANGA YAPONGEZA UAMUZI WA KUVULIWA UONGOZI KATIBU MSAIDIZI
SIKU Chache baada ya Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Taifa (Chadema) kuamua kumvua uongozi ndani ya chama hicho aliyekuwa
katibu Msaidizi Zitto Kabwe chama hicho mkoani hapa kimeipongeza hatua hiyo kwa
kusema italeta umakini mkubwa kwa viongozi waliobaki.
Uamuzi huo ulitolewa kwa mujibu ibara ya 7.7.16 kifungu (V) ambayo
inaeleza kuwa kamati hiyo ina mamlaka ya kumwachisha ujumbe wa kamati kuu
mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume cha katiba, kanuni na maadili au kushindwa
kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
Akizungumza na Tanga Raha,Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga,Jonathan
Bahweje alisema suala hilo lilipaswa kufanywa na kamati hiyo kwa sababu ni
sahihi kwa mtu yoyote anayekiuka kanuni na taratibu za uongozi ndani ya chama
hicho.
Bahweje alisema hatua ya Zitto kukiri kuwa alikosea na
kupewa adhabu ya siku kumi na nne kujitetea kwa kamati kuu ya chama hicho
alitumia busara kubwa sana
na kuwataka wanachama kuwa na utulivu wakati mchakato huo ukiendelea.
“Maamuzi ya kamati
kuu yaliyofanywa sidhani kama yanaweza kuingiliwa na upande mwengine hivyo
napenda kuwaasa viongozi wa ngazi za chini kuacha kuingilia suala hilo kwani tayari
limeshapata muafaka “Alisema Bahweje.
Alisema wanaiomba kamati kuu ya chama hicho kumaliza mgogoro
uliopo huo mapema ili kuweza kujiandaa na uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa
mwaka 2014 kwani wamedhamiri kuhakikisha
wanashinda katika chaguzi hizo.
Katibu huyo aliitaka kamati hiyo kukemea viongozi ambao
wanapiga maamuzi yao
kwani wao ndio chombo cha mwisho ambacho kinauwezo wa kufanya jambo lolote
ambalo linaweza kuleta mgawanyiko ndani ya chama hicho.
“Naishauri kamati
kutumia nafasi yao
kuwaonya viongozi kuanzia ngazi za chini na kuweza kuleta mshikamano wa pamoja
ambao utaweza kuleta mafanikio katika chama chetu kwani uongozi imara ndio
utakiwezesha kuwatumikia wananchi “Alisema Bahweje
PANGANI YAZINDUA UTARATIBU WA UTOAJI VIBALI SHUGHULI ZA UFUGAJI MDOGO
PANGANI YAZINDUA UTARATIBU WA UTOAJI VIBALI SHUGHULI ZA UFUGAJI MDOGO
Wilaya ya Pangani imezindua rasmi cha kitabu cha utaratibu wa
utoaji wa vibali vya shughuli za ufugaji mdogo wa viumbebahari ambao utawawezesha wakazi wa mwambao wa pwani kufanya shughuli za uzalishaji mali bila kuathiri mazingira.
Kitabu hicho kilichozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Hafsa Mtasiwa hivi karibuni kikiwa kimeandaliwa na mradi ujulikanao “Pwani Project”kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho,Mkurugenzi wa mradi wa Pwani,Baraka Kalangahe alisema yaliyoandikwa ni hali halisi ya sasa ya ufugaji mdogo wa viumbebahari na matatizo yanayoikabili tasnia ya maendeleo ya ufugaji mdogo wa viumbe bahari katika Wilaya ya Pangani.
Mengine yaliyoandikwa ni taarifa muhimu za maeneo yanayofaa kwa ufugaji mdogo wa viumbebahari katika Wilaya ya Pangani, maeneo yanayofaa kwa vijiji vya Buyuni, Mkwaja, Mikocheni, Sange,Kipumbwi, Mikinguni,Stahabu,Ushongo Bweni , Mkwajuni, Pangani Magharibi, Mwembeni,Msaraza na Kigurusimba.
Mkurugenzi huo pia alisema Kitabu hicho kinatoa mwongozo wa utoaji wa vibali, ufuatiliaji na udhibiti.
Akizungumza baada ya kuzindua kitabu hicho,Mkuu wa Wilaya alisema mradi huu utasaidia kuongeza thamani ya bahari nakuonya kuwa mtendaji atakayesababisha kuzorota katika eneo lake atamuwajibisha.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA NCHI WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA VIWANDA VYA UTENGENEZAJI NGUO KWA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA (CAPA)
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA NCHI WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA VIWANDA VYA UTENGENEZAJI NGUO KWA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA (CAPA)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Nchi Wanachama wa
Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji Nguo kwa nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC
jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Kinyago kutoka kwa Makamu wa Mwenyekiti wa CAPA wa
Kanda ya Afrika Magharibi, Prof. Daniel Nyarko, baada ya kufungua rasmi
Kongamano la Nchi Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji
Nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza
leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(wa nne kushoto), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru
Kawambwa (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya CAPA,John Kondoro
(kushoto kwa Makamu) na baadhi ya viongozi wa CAPA, wakifurahia kwa
pamoja baada ya kuzindua rasmi Jarida la Wanachama wa Shirikisho la
Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola
Barani Afrika (CAPA Journal), wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo
lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano hilo, wakiwa makini kumsikiliza Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati alipokuwa akisoma hotuba ya ufunguzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia burudani ya ngoma ya Kimasai, wakati akitoka kwenye Ukumbi
wa AICC, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Wanachama wa Shirikisho la
Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola
Barani Afrika (CAPA Journal)lililoanza leo katika jijini Arusha. Picha
na OMR