PANGANI YAZINDUA UTARATIBU WA UTOAJI VIBALI SHUGHULI ZA UFUGAJI MDOGO
Wilaya ya Pangani imezindua rasmi cha kitabu cha utaratibu wa
utoaji wa vibali vya shughuli za ufugaji mdogo wa viumbebahari ambao utawawezesha wakazi wa mwambao wa pwani kufanya shughuli za uzalishaji mali bila kuathiri mazingira.
Kitabu hicho kilichozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Hafsa Mtasiwa hivi karibuni kikiwa kimeandaliwa na mradi ujulikanao “Pwani Project”kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho,Mkurugenzi wa mradi wa Pwani,Baraka Kalangahe alisema yaliyoandikwa ni hali halisi ya sasa ya ufugaji mdogo wa viumbebahari na matatizo yanayoikabili tasnia ya maendeleo ya ufugaji mdogo wa viumbe bahari katika Wilaya ya Pangani.
Mengine yaliyoandikwa ni taarifa muhimu za maeneo yanayofaa kwa ufugaji mdogo wa viumbebahari katika Wilaya ya Pangani, maeneo yanayofaa kwa vijiji vya Buyuni, Mkwaja, Mikocheni, Sange,Kipumbwi, Mikinguni,Stahabu,Ushongo Bweni , Mkwajuni, Pangani Magharibi, Mwembeni,Msaraza na Kigurusimba.
Mkurugenzi huo pia alisema Kitabu hicho kinatoa mwongozo wa utoaji wa vibali, ufuatiliaji na udhibiti.
Akizungumza baada ya kuzindua kitabu hicho,Mkuu wa Wilaya alisema mradi huu utasaidia kuongeza thamani ya bahari nakuonya kuwa mtendaji atakayesababisha kuzorota katika eneo lake atamuwajibisha.
Post a Comment