Kigoda: Kamanda wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM)
WAZIRI wa Biashara na Viwanda
nchini, Dr.Abdalla Kigoda ameteuliwa kuwa kamanda wa Umoja wa Vijana Mkoa wa
Tanga (UVCCM) katika uteuzi ambao ulifanywa na kamati ya utekelezaji Taifa
chini ya Mwenyekiti wao Sadifa Juma.
Akizungumza na Tanga Raha, katika ofisi
za Umoja huo mkoani hapa, Mwenyekiti wa Umoja huo, Abdi Makange alisema
mchakato huo ulianzia ngazi ya mkoa ambapo wao waliamua kumpendekeza Kigoda na
hatimaye kupata baraka kutoka kamati ya utekelezaji na kumuidhinisha kwa
kumpitisha.
Makange alisema hatua yao ya kumpendekeza ilitokana na mchango wake mkubwa aliokuwa ukitolewa na kiongozi huo kwa vijana wa mkoa wa Tanga kitendo ambacho kimewapa wigo katika ufanisi wao.
“Naishukuru sana kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa
kuridhia mapendekezo hayo na sasa tunakwenda kufungua ukurasa mpya wa mafaniko
ndani yetu “Alisema Makange.
Alisema umoja huo unatarajiwa
kuandaa taratibu za kumsimika rasmi kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Handeni mkoani Tanga lengo likiwa ni kuhakikisha wanatimiza malengo yao waliojiwekea.
Post a Comment