MATUKIO YA MAAFALI YA KWANZA YA SHULE YA SEKONDARI ELOHIM YA JIJINI TANGA.
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO KULIA AKIPATA MAELEKEZO KUTOKA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ELOHIM LEO. |
MKURUGENZI WA SHULE YA SEKONDARI ELOHIM YA TANGA,ELINGAYA MUNGURE AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAHAFALI HAYO. |
WANAFUNZI WANAOHITIMU WAKISAKATA LUMBA . |
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO AKIONGOZA HARAMBEE KWENYE SHULE HIYO |
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO ALIZUNGUMZA WAKATI AKITOA HOTUBA YAKE KWENYE MAHAFALI HAYO LEO |
WANAFUNZI WANAOMALIZA WAKIIMBA WIMBO WA TAIFA LEO HII |
Na Lodrik Nowi, Tanga.
Mkuu wa wilaya ya tanga Bi.halima dendegu
ametoa agizo kwa mkurugenzi mtendaji kuhakikisha kuwa ndani ya siku kumi na nne
barabara itokayo chalinze tanga kuelekea shule ya sekondari ya Heloim iwe
imetengenezwa kwa kiwango kizuri.
Agizo amelitoa wakati akiweka jiwe la
msingi iliyokwenda sambamba na mahafali
ya kwanza ya kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya heloim.
Mbali na kutoa agizo hilo Dendegu
ameahidi kutoa vitanda nane kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ili kuweza
kuboresha mazingira mazuri kwa wanafunzi na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Kwa upande wao wazazi wa watoto wanaosoma
ktk shule hiyo wamechangia fedha kwaajili ya vitanda viwili, na kuhaidi
kuendelea kutoa ushirikiano wa hari na mali kwa uongozi wa shule hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo
Bw.geofrey makanza amesema kuwa changamoto
inayowasumbua ni wazazi kutolipa ada kwa wakati pamoja na baadhi ya wanafunzi
kutojitambua kitaaluma.
Aidha mkurugenzi wa shule hiyo
Bi.Elingaya Mungure ameiomba serikali iweze kushirikiana na shule hiyo shule
bega kwa bega ili kufikia malengo ya elimu bora kwa kila mtanzania.
Post a Comment